4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: search > Joel Sebunjo
Results: 1 to 1 of 1
  • Joel Sebunjo

    Country  Uganda
    Genres fusion traditional
    Website /joelsebunjo
    FestivalSauti za Busara 2010, 2014
    Recordings📼

    GANDA MANDE CROSSROADS (2010)

    HEART OF A GRIOT (2011)

    I SPEAK LUGANDA (TBR 2013)

    Joel Sebunjo
    Joel Sebunjo

    Joel Sebunjo alizaliwa mwaka 1984 nchini Uganda, ni kijana mwenye kipaji cha upigaji wa ala tofauti za muziki ambapo vyomba vya habari nchini Uganda vinamfananisha kama Youssou N'Dour wa Uganda. Akiwa sambamba na kundi lake Sundiata wakichanganya ngoma mbalimbali za asili ya Uganda, Gambia, Mali na Senegal.Joel alikwenda Uganda na kugundua mapenzi yake na muziki wa kiafrika. Senegal ndipo alipopata kuona Kora, kifaa chenye asili ya Afrika Magharibi, kimetengenezwa kwa kalabash, nyuzi 21 na kikinakshiwa ngozi ya N'gombe, uchanganyaji wa Sauti za Kora, Gitaa, Kalabash hutoa mdundo na radha halisi ya kiafrika. Ingawa hupiga ala tofauti lakini kwa sasa amekuwa mpiga Kora maarufu. Wanamuziki wanamuelezea kwamba amehamisha ala ya Afrika Magharibi na kuileta Afrika ya Mashariki. Ukimsikia anapoimba basi utajua kwamba nyimbo za Afrika zinaimbika pamoja na haijalishi asili ya nyimbo yenyewe.Anapanda kwa kasi katika medani ya muziki duniani, na ameshapanda jukwaani na majina makubwa katika tasnia ya muziki duniani kama Miriam Makeba, Oliver Mtukudzi, Etran Finatawa, Salif Keita, Baaba Maal, Khaled na wengineo wengi?.