4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: search > Kidumbaki JKU
Results: 1 to 1 of 1
  • Kidumbaki JKU

    Country  Zanzibar
    Genres coastal roots
    FestivalSauti za Busara 2012
    Kidumbaki JKU
    Kidumbaki JKU

    Kidumbaki ni maarufu sana katika kisiwa cha Unguja na moja kati ya ngoma zenye asili ya Zanzibar. Kikundi cha JKU kilianzishwa rasmi mwaka 2000 na kufanikiwa kuongeza sifa zake kila mwaka na sasa kuwa kikundi maarufu sana katika vitongoji vyote vya Zanzibar kwa kila umri kutokana na aina yao ya uchezaji ambayo hunogeshwa kwa kutumia kiuno.

    Kidumbaki hupendwa na watu wengi, katika sherehe za harusi, sherehe za siku za kuzaliwa na sherehe nyingine tofauti muimbaji huimba kutokana na tukio husika. Kidumbaki kinaweza kupigwa kuanzia saa moja mpaka saa nne au tano kwa kuunganisha nyimbo na kivutio kikubwa pale muimbaji anapoimba na watazamaji kuitikia.

    Kidumbaki cha kisasa hutumia nyimbo za taarabu zenye kupendwa. Tofauti na taarab, kidumbaki hutumia sana mtiririko wa utunzi kuliko ushairi wa nyimbo za taarab, mara nyingi huwakosoa watu kuhusu upotofu wa maadili. Katika ujumbe , wanatunga mashairi kutokana na sherehe husika na kutuma ujumbe maridhawa kwa jamii.