4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: search > Kiki Kidumbaki
Results: 1 to 1 of 1
  • Kiki Kidumbaki

    Country  Zanzibar
    Genres kidumbak taarab traditional
    Website www.zanzibarmusic.org
    FestivalSauti za Busara: 2015
    Kiki Kidumbaki
    Kiki Kidumbaki

    Katika miaka ya 1950 sehemu nyingi za Zanzibar ikiwemo mitaa ya Mji Mkongwe kulikuwa na angalau kikundi cha Taarab  au Kidumbaki. Kwa bahati mbaya vimebaki vichache mno. Hata hivyo katika kijiji cha Mahonda nje ya Mji Mkongwe, njia ya kuelekea Kaskazini mwa Kisiwa cha Unguja, ndipo panapopatikana kikundi cha KIKI KIDUMBAKI kilichoanzishwa tangu mwaka 1993.
    Miaka kumi iliyopita kiongozi wa Kikundi, marehemu Ali Baramia alimfuata Hilda Kiel ambaye alikuwa kiongozi wa Chuo cha Mziki Zanzibar (DCMA) alimuomba msaada wa kuendeleza sanaa ya mziki kwenye kikundi. Matokeo yake palifunguliwa tawi la Chuo cha Mziki (DCMA) chini ya udhamini wa UNESCO kwa kusaidia kufundisha walimu na wasanii na kununua vifaa na kufanyia matengenezo ya jengo la chuo na mahitaji mengine. Katika hali hiyo KIKI TAARAB kiliweza kufanya maonyesho yake mara nyingi ndani ya DCMA, Mji Mkongwe na Mahonda lakini tangu udhamini ufikie kikomo DCMA ilikuwa inahangaika kutafuta pesa kwa ajili ya kukiendeleza kikundi.
    Kwa bahati nzuri wasanii waliweza kukiendeleza kikundi. Mkurugenzi wa Sanaa wa DCMA, Matona Mohammed anajitahidi kuboresha uwezo wa kufanya maonyesho kwa vikundi vyote vya DCMA. Katika hali hiyo kikundi kinafanya maonyesho ya kila wiki sehemu mbalimbali kama Old Dispensary, Gymkhana Club, na baadhi ya maeneo ndani ya Mji Mkongwe. KIKI kimefanikiwa kujizolea sifa ya kuwa kikundi bora cha Kidumbaki tofauti na vikundi vingine vinavyopunguza radha asilia za kidumbaki.