4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: search > Kozman Ti Dalon
Results: 1 to 1 of 1
  • Kozman Ti Dalon

    Country  Reunion
    Genres acrobats traditional
    Website /kozmantidalon
    FestivalSauti za Busara 2012
    Recordings📼

    A Ou Pépé (2005); Ti Fler Flambo (2008); La Tribu Des Sakalava (2011)

    Kozman Ti Dalon - Clip Bambo (2011)

    Kozman Ti Dalon
    Kozman Ti Dalon

    Kozman Ti Dalon ni kikundi cha vijana sita machachari kutoka katika kisiwa cha Reunion ambao wanaishi kwa kutemea muziki wao na utamaduni wao. Wote wamezaliwa ndani ya Reunion katika mji wa Saint Louis. Walipata msukumo kutoka kwa mwanzilishi wa aina ya muziki wa maloya kabaré marehemu Granmoun Bébé. Albamu yao ya kwanza waliitoa mwaka 2005 na kuipa jina la Gras a ou pépé ikiwa ni sifa kwake.

    Kozman Ti Dalon wanawakilisha vyema kizazi kipya cha muziki wa Maloya na kuupa heshima urithi wa muziki wa maloya na kutaka kuusambaza dunia nzima. Muziki wao wa utamaduni ambao unatumia vifaa mbalimbali.

    Kikundi kinaongozwa na Jonathan Camillot, ni mwimbaji na mjukuu wa Gramoun Bébé Manet. Shauku ya vijana kuhusu muziki wa maloya, Jonathan alikutana na ndugu zake na kuunda kundi lao katika miaka ya 90. Tangu hapo Kozman Ti Dalon iliendelea kutekeleza ahadi zake za kuutangaza mauziki wa Maloya kila sehemu waendayo, wameshafanya maonyesho makubwa nyumbani kwao Reunion, Kanada, Ufaransa na katika visiwa vya Bahari ya Hindi.

    Maonyesho yao yana sifa ya muziki wa Maloya, watafanya maonyesho katika tamasha la Sauti za Busara 2012 katika maandamano na ndani ya steji ya Ngome Kongwe. Usikose kuwaona wakifanya maonyesho yao ya nguvu na uchangamfu.

    Kozman-travel-sponsors
    Thanks to Department of Reunion and Region Reunion