4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: search > Leo Mkanyia and the Swahili Blues Band
Results: 1 to 1 of 1
 • Leo Mkanyia and the Swahili Blues Band

  Country  Tanzania
  Genres band jazz traditional fusion
  Website www.leomkanyia.com
  FestivalSauti za Busara: 2012, 2015
  Recordings

  Dunia Hii (2010); Jasho Langu (2011)

  Jasho Langu Music Video

  Leo Mkanyia and the Swahili Blues Band
  Leo Mkanyia and the Swahili Blues Band

  Biyi Adepegba, Muongozaji msanifu wa Joyful Noise Recordings Uingereza na London African Music Festival ameelezea muziki wa Leo Mkanyia kama ‘muziki wa bluzi unaokumbushia maajabu ya Mfalme wa Muziki wa bluzi Afrika Ali Farka Toure. Rachel Boyle wa New York Times alivutiwa na ‘mchanganyiko wa ngoma za Kitanzania na milio ya kibluzi na dansi’. Hii ni aina yake ya kipekee na ya kisasa ya Leo Mkanyia ambayo anaiita Swahili Blues. Leo Mkanyia amethubutu kutofanya muziki unaotawala katika vyombo vya habari, nje ya boksi la muziki maarufu. Amejipatia sehemu yake na ana wafuasi mashabiki maradufu ambao ni wa ndani ya nchi na kimataifa.
  Leo alizaliwa Dar es Salaam mwaka 1981. Alianza kupiga gitaa akiwa na umri wa miaka nane tu. Baba yake ni mpiga gitaa wa aina ya muziki wa African Jazz katika bendi mashuhuri ya Mlimani Park Orchestra. Leo alitumia miaka mingi akipiga gitaa ya baba yake akiwa peke yake nyumbani, huku akifuata mpangilio wa sauti aliokua akipiga baba yake. Muziki haulipi Tanzania, hivyo baba yake Leo alimkamia mwanae atafute kazi tofauti lakini siku moja alipomkuta Leo akipiga nyimbo moja ya zamani ya Kitanzania, aliamua kumpa mwanae ndoto yake na kumfundisha mambo yote aliyokua akifahamu.
  Hivi leo wanapiga muziki pamoja, huku Leo akiongoza bendi na baba yake akipiga gitaa aina ya solo. Mnamo mwaka 2010 Leo alirekodi CD ya nyimbo 4, aliyoipa jina “Dunia Hii”. Leo aliachia albamu yake kamili mwezi wa nane mwaka 2011, “Jasho Langu”, ambayo ilipata uchambuzi mzuri sana. “Hivi sasa namalizia albamu mpya ambayo itatoka miezi inayokuja” alisema.
  Leo ameshafanya maonyeshio matamasha mbalimbali kama London African Music Festival mwaka 2011, Sauti za Busara mwaka 2012 na Bayimba Festival, Uganda mwaka 2013.
  Nyimbo za Leo ni zenye hisia kali; zinaonesha maisha halisi ndani ya Tanzania. Nyimbo zake zinasherehekea historia na tamaduni za Tanzania na Afrika kwa ujumla, zinaelezea hadithi ya uhamiaji kutoka kijijini kwenda mjini, uwiano wa kijinsia pamoja na uwezeshaji kwa wanawake, siasa na utawala mbovu pamoja na mapenzi. Katika muziki wake utasikia nyimbo maarufu za zamani za Kitanzania, muziki wa dansi (zilipendwa) lakini ukiwa na msokoto wa muziki wa kisasa, bluzi na afrobeat. Zote zikiwa ni uwakilishi wa muziki bluzi asilia wa Tanzania, aina ya muziki ambao Leo anakazania ili utunzwe.