Results: 1 to 1 of 1
Les Frères Sissoko
Country Senegal Genres acoustic roots traditional Festival Sauti za Busara 2011 Bao na Sadio Sissoko walizaliwa toka katika familia ya wanamziki “wakongwe” wa huko Senegali wanamziki hawa wawili walianza kupiga chombo cha kisenegali kijulanacho kama kora tangu wakiwa na umri mdogo wa miaka saba pamoja na hilo. Wanamziki hawa vilevile ni wajuzi wa upigaji magitaa, ngoma, violini na saxophone. Kwa sasa wanaishi nchini Ubeligiji. Les Freres Sissoko kama bendi huchanganya mziki wa asili wakisenegali ambao unatokea katika kabila la Mandingo mchakato huo wakimziki ni kutoka mtindo kama Reggae, Jazz, Zouk na Salsa. Pamoja na kwamba Mziki wao una msukumo mkubwa kutoka katika utamaduni wakisenegali vyombo vya kisasa wanavyovitumia vimeongezea vionjo vya aina yake. Huku wakiongezea nguvu na Komlan Octave katika ngoma na Wouter Van den Abeele apigae violin wanaziki hawa wanne pamoja wanatarajia kutoka burdani yakipekee wafikapo Zanzibar.
With thanks to Communaute française Wallonie-Bruxelles