4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: search > Liza Kamikazi and band
Results: 1 to 1 of 1
 • Liza Kamikazi and band

  Country  Rwanda
  Genres acoustic traditional fusion
  Website www.lizakamikazi.com
  FestivalSauti za Busara: 2015
  Recordings

  Hobeee(2009); Iy'Iwacu (2011)

  Liza Kamikazi and band
  Liza Kamikazi and band

  Liz Kamikazi ni mwimbaji, mtunzi na muigizaji. Alipata mafunzo yake ya uigizaji katika Kituo cha Sanaa katika Chuo kikuu cha Rwanda, ambapo alimaliza na shahada ya Mawasiliano. Mwaka 2013 Liza alizindua albamu ya Iwacu nyumbani hapo. Mwezi wa pili mwaka huo huo alitumbuiza na bendi yake katika tamasha na Panafrican Festival of Dance (Fespad) pamoja na Jamafest, tamasha jipya Afrika Mashariki nchini Rwanda. Nyimbo zake Kigali na More than a dream zilichaguliwa kuwania tuzo za East African Music Awards mwaka 2011. Mwaka 2011 alifanya maonesho nchini Canada. Huko Demokrasia ya Congo, alitumbuiza katika tamasha la Bukavu Participatory Theater Festival na tamasha Uvira. Alikua muigizaji mkuu katika filamu fupi We Are All Rwandans iliyotengenezwa na mtengeneza filamu wa Uingereza Debs Gardner, na nafasi nyingine alicheza katika filamu ya kifaransa Zone Turquoise. Liza Kamikazi anaimba miondoko ya afro-fusion. Kimuziki, vipaji vya Liz vilimpeleka Nairobi ambapo alirekodi na kuzindua album yake ya kwanza Hobeeee mwaka 2010. Vile vile aliachia nyimbo katika redio za ndani ya nchi, na ngoma ya Usiniache Baby ilikua maarufu Afrika Mashariki yote. Liz alitunga muziki kwa maonesho ya kitaifa kama vile Miss Rwanda 2009, sherehe za kila mwaka za maadhimisho ya siku ya kitaifa ya ukombozi wa Rwanda. Vile vile amefanya maonesho na watoto katika sherehe za kijamii juu ya masuala ya ufahamu. Liza ni mmoja wa waanzilishi wa Kaami Arts, shirika ambalo linaendeleza sanaa kwa watoto. Mwaka 2014, Liza alitunga Urumuru Rutazima, nyimbo maalum ya kuadhimisha miaka 20 ya mauaji ya kimbali ya Rwanda. Iliimbwa na vikundi tofauti vya watoto katika wilaya 30 za Rwanda na kufikia kiwango katika onesho lililojumuisha waigizaji 1,000 katika uwanja wa taifa siku ya ufunguzi wa sherehe hizo.