4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: search > Lumumba Theatre
Results: 1 to 1 of 1
  • Lumumba Theatre

    Country  Tanzania
    Genres acoustic band dance fusion
    FestivalSauti za Busara 2012, 2013

    Lumumba Theatre
    Lumumba Theatre

    Lumumba Theatre ni kikundi chenye vijana wenye vipaji katika fani uimbaji, uigizaji na muziki. Lumumba ilianzishwa mwaka 1997 na kiongozi wa kundi hilo Djuto Komba alianza na kuwakusanya vijana wenye vipaji kutoka katika Shule ya Msingi ya Lumumba iliyopo maeneo ya Mnazi mmoja ndani ya jiji la Dar es Salaam. Lumumba wanauchu wa mabadiliko na maendeleo ya kijamii. Katika kulishughulikia hilo wanahamasisha vijana kwa kutoa mafunzo ya uchezaji ngoma, maonyesho na muziki, na kutoa nafasi kwa vijana kusoma, kuonyesha ubunifu wao na kuufanyia kazi. Lumumba wameshafanya maonyesho nchi mbalimbali kama Kenya, Uganda, Msumbiji, Ujerumani, Denmak, India na Poland.

    Kipindi cha mwanzo waliangazia ngoma za asili za Tanzania, kwa sasa wamefanya mseto wa shughuli tofauti na kutoa semina ya uchezaji, kuandaa maonyesho, uandishi wa hadithi na muziki wa Afrika.

    Wanatumia vifaa tofauti kama Sexaphone, Filimbi, Marimba, Kinanda na Gitaa, na ni kikundi chenye nidhamu, uzoefu katika ngoma za asili na za kisasa. Huwa hawachoshi kuwaangalia wawapo jukwaani na kuhakikisha kila mtu anaridhika na wanachokifanya.

    Walifanya onyesho la nguvu katika tamasha la busara 2012 na umati wa watu uliwashangalia na kusema wameleta changamoto kwa vikundi vya Tanzania.