4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: search > Lydol
Results: 1 to 1 of 1
 • Lydol

  Country  Cameroon
  Genres acoustic spoken word
  Facebook /LydolSlam
  FestivalSauti za Busara 2019
  Recordings

   Slamthérapie, 2018 

  Lydol - Light (official video)

  Lydol
  Lydol

  Nwafo Dolly Sorel, aka Lydol alizaliwa jijiini Yaoundé mwaka 1994. Alijihusisha na muziki na utamaduni wakati akiwa shule ya sekondari. Mwaka 2010 alishinda tuzo ya taifa katika kipengele cha slam. Kuanzia hapo alianza kufanya maonyesho katika Taasisi ya Goethe Institut, Kituo cha Utamaduni Camerounais na maeneo mengine ya jiji. Mwaka 2013, Lydol iliwakilisha Kameruni nchini Angola katika Spoken Word Project, na mwaka uliofuata alishiriki kwenye tamasha la mashairi nchini Afrika Kusini.

  Tangu mwaka 2015, kwa ushirikiano na Taasisi ya Goethe nchini Cameroon, Lydol imekuwa kushiriki katika kuandaa Sayansi Slam Cameroun. Pia huanda warsha za uandishi “Style Haut-Pen" na kuongoza majaji wa Slam Party katika mashindano ya shule.

  Lydol alitoa albamu yake ya kwanza 'Slamtherapie' mwezi Aprili 2018. Mradi wake katika slam haikuwa uamuzi wa kisomi, lakini mudaulivyozidi kwenda aligundua kwamba kazi yake inaweza kuwekwa kwenye kundi hilo. Anapenda kushirikiana na kuipigania Slam iweze kwenda mbele zaidi katika mambo ya warsha. Lydol ni shabiki wa muziki wa jukwaani, maonyesho, ngoma na soka. Lydol ana PhD baada ya kumaliza Master of Degree ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha Yaounde.