4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: search > Mabantu Africa
Results: 1 to 1 of 1
  • Mabantu Africa

    Country  Tanzania
    Genres traditional fusion hiphop bongo flava
    Website www.wakupetimusic.blogspot.com
    FestivalSauti za Busara: 2015
    Recordings📼

    Muziki wa Sasa (2013); Nimuite Nani (2014); Kabla Jua Kuzama (2014)

    MaBaNtU njoo hUkU directed by abou the deal

    Mabantu Africa
    Mabantu Africa

    Mabantu Africa ni bendi ambayo iliundwa na vijana wawili Kitanzania, Creator na Twaah wenye umri wa miaka 16 na 17. Wote wamebarikiwa kuwa na vipaji vyenye nguvu katika kutunga na kutumbuiza muziki. Wakiwa wenyeji wa kijiji cha Nachingwea katika Mkoa wa Mtwara, walianza kuimba wakiwa katika kwaya ya shule ya msingi. Wakiwa bado wadogo, walitoroka kijijini na kuhamia Dar es Salaam, wakitafuta fursa bora. Lakini maisha mjini hayakua kama walivyoyafikiria; maisha yalikua ya shida na hawakua na sehemu ya kuishi, hawakuwa na chakula wala pesa. Mwishowe waliamua kuomba nafasi ya kujiunga katika kituo cha watoto cha Mkubwa na Wanawe kilichoanzishwa na Said Fela, promota maarufu wa muziki ili waweze kuendeleza vipaji vyao.
    Kituo hicho cha Mkubwa na Wanawe kiliwapa vijana hawa sehemu ya kupumulia ambayo walikua wakihitaji, wakati huo huo wakitazama na kujifunza jinsi ya kukabiliana na maisha ya jijini. Mnamo mwaka 2013 waliamua kujitoa katika Kituo hicho na kuunda kundi lao wenyewe. Hivyo Mabantu Africa ikazaliwa, huku Creator na Twaah wakiwa wenye kujiamini zaidi katika muziki na kusafiri katika mikoa tofauti tofauti Tanzania kutumbuiza. Waliamua kuunda kundi la Mabantu kama kutoa heshima kwa kabila kubwa Mkoani Mtwara ambapo Wamakonde ni wajuzi katika sanaa. Mabantu Africa hivi sasa wanafanya kazi chini ya Wakeputi Music Recordz (WMB). Kama wasanii wengine wengi katika tasnia ya muziki wa Bongo flava, Mabantu Africa hutumbuiza kwa ‘playback’. Hivi sasa wako bize wakijiandaa na bendi kwa ajili ya kutoa burudani ya nadra na maalum katika Sauti za Busara 2015, 100% live!