4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: search > Mani Martin
Results: 1 to 1 of 1
 • Mani Martin

  Country  Rwanda
  Genres acoustic band pop fusion
  Website www.manimartin.com
  FestivalSauti za Busara 2013
  Recordings

  Isaha ya Cyenda, 2007; Icyo Dupfana Kiruta Icyo Dupfa, 2010; Intero y’Amahoro, 2011; My Destiny, 2012

  MANI Martin -INTERO Y'AMAHORO (OFFICIAL MUSIC VIDEO)

  Mani Martin
  Mani Martin

  Mani Martin alizaliwa mwaka 1998 magharibi mwa Rwanda, alipofikia umri wa miaka tisa kipaji chake kilianza kuonekana alipokuwa anaimba shuleni. Mwaka 2000 alipokuwa ana umri wa miaka 11 alifanikiwa kurekodi nyimbo 12 za kwaya na kuwa maarufu katika makanisa mengi nchini Rwanda.

  Kama kawaida kwa wanamuziki wengi huvutiwa na baadhi ya wasanii wenzao, kwa Mani Martin alivutiwa na Cecile Kayirebwa, Jean Paul Samputu, Ismail Lo na R Kelly. Nyimbo yake ya kwanza iliyompatia umaarufu nchini Rwanda na nchi jirani ilijulikana kwa jina “Urukumbizi” ambayo ilifanikiwa kupata tuzo ya nyimbo bora ya mwaka 2006. Mwaka huohuo Mani alichaguliwa kuwa mwanamuziki kijana na kuiwakilisha Rwanda FESPAD.

  Mani anaimba lugha tofauti kama Kinyarwanda, kingereza, Kiswahili na kifaransa ambapo hufanya maonyesho yake kwa mchanganyiko wa vifaa za asili na vya kisasa.

  Albam ya kwanza aliipa jina la “Isaha ya Cyenda” ambayo aliitoa mwishoni mwa mwaka 2007. Alipata tuzo ya kuwa mwanamuziki bora wa kiume mwaka 2007 na mwaka 2008 alizawadiwa tuzo ya Salax ya mwanamuziki bora wa kiume wa kwaya.  

  Mwaka 2010 alitoa albam ya pili aliyoipa jina “Dupfana Kiruta lcyo Dupfa” ambayo iliangazia suala la amani, umoja na maridhiano. Mani Martin amapata umaarufu na mara kwa mara anaiwakilisha Rwanda katika mikutano na matamasha mbalimbali ndani na nje ya nchi.  

  Kipaji cha Mani Martin kimekuwa zaidi baada ya kushiriki katika filamu ya “Long Coat” ambayo ilikuwa inaelezea ukatili na manyanyaso ya watu wa Rwanda. Katika tasnia ya muziki wa Rwanda Mani anafahamika kama muimbaji wa Pop na R&B kutoka katika lbamu yake ya tatu ya “Intero y’Amahoro”

  Albamu ya nne ambayo ameitoa hivi karibuni aliyoipa jina la “My Destiny” ndani yake amechanganya muziki wa asili na wa kisasa.