4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: search > Mashauzi Classic Modern Taarab
Results: 1 to 1 of 1
 • Mashauzi Classic Modern Taarab

  Country  Tanzania
  Genres band coastal pop
  FestivalSauti za Busara 2012

  Mashauzi Classic Modern Taarab - Mama Mashauzi (Official Video)

  Mashauzi Classic Modern Taarab
  Mashauzi Classic Modern Taarab

  kundi la mashauzi classic ni moja kati ya makundi maarufu Tanzania bara na visiwani katika tasnia ya muziki wa taarabu ya kisasa (Modern Taarab)

  Ilianza kupata umaarufu katika miaka ya 1990, kilikuwa kilio cha muda mrefu kutoka kwa wanamuziki wa zamani wanaopiga taarab asilia na wakilalimika kwamba hii sio taarab. Lakini bado iliendelea kupata umaarufu na kupendwa hasa na wanawake kutokana na ujumbe na midundo yake inayohamasisha kucheza.

  Mashauzi Classic Modern Taarab ilianzishwa mwaka 2011 na wanamuziki maarufu wawili, Isha Ramadhan na Thabit Abdul ambao walifanikiwa kuvuta hisia za mashabiki wao kwa haraka kutokana na mfumo wa uimbaji na uchezaji.

  Isha Ramadhan maarufu Isha mashauzi, safari yake ya muziki amepitia vikundi tofauti ikiwemo  Segere Original. Aalijiunga na Jahazi Modern Taarab mwaka 2007 kutokana na ushauri wa mzee Juma Mbizo, alianza kutambulika katika tasnia ya taarab ya kisasa alipoimba mwimbo wa kwanza “Hayanifiki” na “Yawenzenu Midomoni”. Mwaka 2010 alofanikiwa kutoa albamu yake mwenyewe aliyoipa jina “Mama nipe radhi” katika mwaka huo Thabit Abdul alijiunga na Jahazi Modern Taarab na ndipo walianza matayarisho ya uzinduzi wa kundi lao, ambalo kwa sasa linajulikana kama Mashauzi Classic. Thabit Abdul ni mpaga kinanda maarufu Tanzania na amepitia bendi tofauti ikiwemo Extra Bongo, All Star Modern Taarab, TOT, Jahazi Modern Taarab na African Stars Band (Twanga Pepeta).