4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: search > Mim Suleiman
Results: 1 to 1 of 1
 • Mim Suleiman

  Country  Zanzibar UK
  Genres urban fusion pop
  Website www.mimsuleiman.com
  FestivalSauti za Busara 2010, 2015
  Recordings

  Tungi (2010); Umbeya (2012)

  Mim Suleiman
  Mim Suleiman

  Ya kubembeleza, ya kupaza, ya kina na ya kimungu, uwepo wa Mim ni baraka.
  Mim Suleiman ameelezwa kuwa “msanii mwenye umbo dogo lakini mwenye haiba kubwa mfano wa sayari”. Anaimba ‘mchanganyiko wa Afro-beat na global fusion’, mara nyingi kwa lugha yake asili ya Kiswahili na wakati mwingine kuchepuka na kutumia Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifulani. Mim Suleiman ana sauti yenye uwezo wa kubadilika badilika, ni msanii mkarimu na machachari. Ukiacha miondoko yake na uwezo wake wa kucheza Mim amebarikiwa sauti kubwa pamoja na haiba yenye bashasha.
  Hivi karibuni alitumbuiza kama mmoja wa wanachama 80 katika tamasha lenye sifa kubwa Uingereza linaloitwa Africa Express train tour of the UK, na katika BT River of Music kama sehemu ya tamasha la pre-Olympic world music festival. Ni msanii aliyerekodiwa na Real World na kuorodheshwa kwenye WOMAD, Mim pia anaendesha warsha za uimbaji pamoja na uwasilishaji wa hadithi..
  Kwa sasa Mim anaandika kitabu kuhusu mapishi, muziki na hadithi za Zanzibar. Akifanya kazi pamoja na mtengeneza filamu Zippy Kimundu, Mim anafanya filamu iitwayo ‘Usista’, anasafiri sehemu mbalimbali za  Afrika Mashariki akikutana na wanawake tofauti wakieleza hadithi zao, ili kutuwezesha kuwa na uelewa tofauti jinsi gani dunia inavyokwenda.
  Mim Suleiman ameachia albam 2 za pekee. Vilevile alikua mwimbaji wa sauti ya nyuma katika albamu iliyoshinda tuzo iliyopewa jina ‘Tell no Lies’ ya Justin Adams & Juldeh Camara (JuJu), na pia alikua mwanachama wa kundi la Sheffield’s Rafiki Jazz.