4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: search > Mpamanga
Results: 1 to 1 of 1
 • Mpamanga

  Country  Madagascar
  Genres roots traditional fusion
  Website /mpamanga
  FestivalSauti za Busara 2015
  Recordings

  Kultur (2011); Maquette Live (2013)

  MPAMANGA Clip Ratanalah

  Mpamanga
  Mpamanga

  Linajumuisha wanamuziki watano wazoefuna ZIX mpiga gitaa la bass na mwimbaji, Jacquis Ralf mpiga gitaa na mwimbaji, Herry mpiga ngoma na pedi, Toky kwenye keyboards na sauti na Beme kwenye percussion na kusababisha sauti; Kundi Mpamanga liko katika game tangu 2009.
  Wasanii  kutoka Antsirabe, kila msanii alikuwa na uzoefu wake sambamba : Jacquis Ralf nilijulikana kama mpiga gitaa la Jazz ; Bema , ZIX na Toky walikuwa waanzilishi wa M'boutah kundi , unaojulikana kitaifa; na Herry alifanya kazi kwa miaka mingi na wasanii wadogo na wa kitaifa kama Injinia wa sauti na mpiga ngoma.  Tangu mwaka 2009, Mpamanga inafanya kazi za kimuziki: kwanza katika mji wa Antsirabe ambapo walijulikana kisha kuelekea katika majukwaa makubwa ya mji mkuu Malagasy Taasisi ya Kifaransa, Circle Germano - Malagasy, Alliance Françaises, Jao’sPub. ), na matamasha makubwa zaidi ya (Angaredona 2011, 2012 et 2013; Mamahoaka 2011, 2012 et 2014 ; Madajazzcar 2011 et 2012, Libertalia Music Festival 2014...).. Kila moja ya matamasha yao ni nafasi nzuri zaidi ya kundi kukua na kuonyesha hisia zao katika jukwaa: kucheza na kuimba na mashabiki , na uwezo wao mkubwa wa kimuziki. Ni moja ya makundi ambayo muziki wao unabaki kichwani kwa muda mfrefu baada ya shoo.  Kundi imetoa albamu yao ya kwanza "To Kultur” mwezi Februari 2011, na tangu wakati huo wanaendelea kuandika na kutunga nyimbo mpya. Wakijikita zaidi katika ulimwengu wa Afro- beat na fusion, muziki wa Mpamanga ufafanuliwa kimsingi kama kundi la muziki mchanganyiko wa Malagasy, sifa ya kikundi. " Mpamanga " maana yake " haswa kuhama hama " kwa Malagasy ; na ni " kuhamahama " kulikofanya kila mwanamuziki katika kundi  kuweka vionjo vyake vya asili ambavyo vimetengeneza muziki wa aina ya kipekee na ya ukweli. Kwa hakiki kucheza pamoja kwa miaka mingi, imesaidia sana kundi la Mpamanga kushikamana, na radhi kucheza pamoja kwa mawasiliano mbele ya washabiki wao. Kila msanii pia ana nafasi maalum ya kuimba peke yake na kuonyesha ujuzi na talanta yake.
  Mpamanga pia wanatoa ujumbe kwa jamii kuhusu utamaduni wa malgache,: nyimbo zao zinaongele maisha ya kila siku ya wamalgache; familia, mapenzi,asili,kazi,maisha ya jamii kwa njia ambayo inaweza kuigusa jamii.
  Mwaka 2014, walikua kati ya wanamuziki kumi waliochaguliwa kushiriki katika tamasha la Libertilia Music ambolo lengo lake ni kukuza wasanii wa malagasy 10 kuchaguliwa kwa kushiriki katika tamasha Libertalia Music, ambayo ina lengo la kukuza wasanii Malagasy katika jukwaa la kimataifa. Programu ya tamasha ni kuonyesha vipaji vya Mpamanga kwa sababu uteuzi wa wasanii unategemea na uwezo wao wa kujirusha katika jukwaa la kimataifa.

   


  Walipata fursa katika tamasha hili ya mafunzo ya kisanii na wataalamu wa Kireunion na Kifaransa. Ujumbe kutoka Alliances Françaises, Madagascar waliwapa pendekezo la kufanya ziara ya kitaifa Alliances Françaises zote nchini Walipewa sifa na maafisa wa Alliances Françaises waliowakaribisha kwa kiwango chao na uwezo wao kimuziki. Leo Mpamanga iko tayari kuvuka mipaka na kutoa muziki wao kwa washabiki wapya.