4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: search > N\'Faly Kouyaté
Results: 1 to 1 of 1
  • N'Faly Kouyaté

    Country  Guinea
    Genres traditional roots fusion
    Website www.nfalykouyate.com
    FestivalSauti za Busara 2008, 2013
    Recordings📼

    N’faly Kouyate & Dunyakan:

    N’na Kandje, 2001; Kora Grooves, 2004; Kora Strings, 2011;

    with Afro Celt Soundsystem:

    Release, 1998; Further in Time, 2001; Seed, 2005

    N'Faly Kouyaté + Dunyakan Love Hyppo

    N
    N'Faly Kouyaté

    N'faly Kouyaté alizaliwa katika mji wa Siguiri na kukulia Conakry mji mkuu wa Guinea. Ameishi barani ulaya tangu miaka ya 90 ambapo amefurahia kazi yake ya usanii na hasa kupitia chombo chake cha Kora ambacho ni maarufu katika nchi za Afrika ya Magharibi, N’faly amefananishwa na “Jimi Hendrix wa Kora”

    Mwaka 1997 alialikwa kujiunga na Fusion Bank Afro Celt Sound System ambayo inachanganya mahadhi ya kiafrika na ki irish, N’faly alikuwa na hiyo bendi na kufanya maonyesho mengi dunia nzima kama Glastonbury, WOMAD, Montreaux and Montreal. Walifanikiwa kutoa albam kadhaa ambapo baadhi zimechaguliwa kupata tuzo za kimataifa. Mwaka 2002 bendi ilifanikiwa kupata tuzo ya chaguo la wasikilizaji cha kituo cha redio BBC 3.

    Ushiriki na wasanii mbalimbali ni moja kati ya mafanikio ya N’faly ambapo mwaka 2008 alifanya onyesho katika Tamasha la Sauti za Busara na kundi lake “Dunyakan” ambalo wambalo wamashafanya maonyesho mengi ndani ya bara la ulaya akiwa kama muimbaji, mtunzi na mpangaji. Almeshashirikiana na wasanii kutoka Guinea, Cameroun, Angola, Ufaransa na Ubelgiji akiambatana na vifaa vyake kama Kora, Balafon, ngoma aina ya jembe, tama na nyinginezo. Muziki wake huchanganya na vifaa vya umeme.

    Katika maonyesho yake hutumia muziki kama njia ya kupeleka ujumbe kwa watu kuhusu tamaduni tofauti, hufanya jitihada za kuelezea kuhusu tamaduni na kuheshimiana, kutengeneza umoja na mshikamano. Hufanya kazi bila ya kuchoka kutetea utamaduni wake, mapenzi yake ni kuungana na kuvumbua ulimwengu mpya.

     

    LOGO_WBI_noir_basse_resolution
    With thanks to Wallonie Bruxelles International