4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: search > Nathalie Natiembe
Results: 1 to 1 of 1
  • Nathalie Natiembe

    Country  Reunion
    Genres band roots fusion
    Website /nathalienatiembe
    FestivalSauti za Busara 2013
    Recordings📼

    Margoz, 2001; Sankèr, 2005; Karma, 2009

    Nathalie Natiembé - Karma

    Nathalie Natiembe
    Nathalie Natiembe

     

    Nathalie Natiembé ni mwanamuziki kutoka katika visiwa vya Reunion, Natiembé alianza kujitambulisha kimataifa kama mwanamuziki mwaka 1997. Natiembé ni muimbaji wa muziki wa Maloya na ni miongoni mwa wanamuziki wenye vipaji vya ubunifu ambapo hufanya jitihada binafsi za kuwakilisha muziki wa maloya na kuuongozea vionjo kutoka kutoka sehemu mbalimbali za dunia kama ndani ya ukanda wa bahari ya hindi, Afrika na Ulaya, huchanya radha zote na kufanikiwa kuupa radha ya kipekee muziki wa Maloya.

    Mwaka 2001 alikwenda Msumbiji aligundua asili ya muziki huu, alifanya utafiti pamoja na wanamuziki watatu kutoka Msumbiji ambao walimruhusu kuangalia muziki tofauti wenye urahisi na ushawishi kwake. Ilijuisha "Jazz, blues, soul, R & B na Muziki kutoka Karibian na Cape Verde".