4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: search > Owiny Sigoma Band
Results: 1 to 1 of 1
 • Owiny Sigoma Band

  Country  Kenya UK
  Genres acoustic roots fusion
  FestivalSauti za Busara 2013
  Recordings

  Owiny Sigoma Band, 2011

  Owiny Sigoma Band - The Luo-London Soundclash

  Owiny Sigoma Band
  Owiny Sigoma Band

  Mwaka 2009 wanamuziki kutoka Uingereza walikwenda nchini Kenya kwa ajili ya kushirikiana na wasanii wenzao wa kenya. Kulikuwa hakuna ajenda maalum zaidi ya kuwakutanisha wasanii, kubadilishana mawazo. Muziki wa Kenya ulikuwa hauna umaarufu kama muziki wa Afrika Magharibi, kusini na Kaskazini kwa hiyo lengo kuu lilikuwa kujaribu kuandaa miundo mbinu. Bendi ikaandaa mazingira ya kuwakutanisha Fela Kuti naTony Allen kwa mapendekezo ya Thomas Mapfumo na Oumou Sangare, na huu ndio ulikuwa mwanzo kwa wanamuziki wa Uingereza Jesse Hackett (kinanda), Louis Hackett (Bess Gitaa), Sam Lewis (Guitaa), Chris Morphitis (bouzouki/guitaa) and Tom Skinner (ngoma) kufika Kenya kwa masuala ya Muziki.

  Mara ya kwanza kufika Kenya ilikuwa mwaka 2009 na kushirikiana na wanamuziki wawili wa kabila la waluo Joseph Nyamungu na Charles Owoko. Mazoezi yao yalikuwa ya kupendeza “Walifanya ni kipindi cha kubadilishana ujuzi na njia ya kushirikiana kimuziki. Tulisoma nyimbo zao na wao walsoma nyimbo zetu”. Alielezea Tom. Upatikanaji wa Studio yenye uwezo wa kuchukuwa watu saba kwa mara moja ilikuwa ngumu, lakini baadae ikapatikana sehemu ya kiwanda isiyotumika na kurekodi.

  Walitoa nyimbo nne na kuzipeleka kwa Gilles Peterson (BBC Worldwide), ambaye maramoja alisaini mkatana na lebo yake “Brownswood record label” na kuirudisha tena bendi Nairobi kwa ajili ya kufanya rekodi na Joseph, Charles na marafiki zao. Mwaka 2011 wametoa albam yao wenyewe.