4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: search > S Kide
Results: 1 to 1 of 1
  • S Kide & Wakupeti Band

    Country  Tanzania
    Genres bongo flava urban fusion
    Facebook /skide.shamte
    FestivalSauti za Busara 2019
    Recordings📼

     Kabla Hajatoka Diamond, 2010; Ushemeji Upo Haliwi Mtu, 2017; Kwetu Mbagala, 2017

    S Kide & Wakupeti Band
    S Kide & Wakupeti Band

    Shamte Mohammed aka S Kide ni mtunzi na mwimbaji wa staili ya singeli. Muziki wa singeli na uchezaji wake umebuniwa katika vitongoji vya Mji Dar es Salaam na katika miaka ya karibuni imezidi kuvutia watu ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.  

    S Kide alizaliwa na kukulia Dar es Salaam. Safari yake ya muziki ilianza wakati alikuwa na umri wa miaka 9 tu. Alikuwa anawakusanya wanafunzi wenzake na kuwaimbia mchiriku wakati wa mapumziko ya shule, na akaanza kupata umaarufu.

    Kutokana na changamoto za kifedha, baada ya kumaliza shule ya msingi hakuweza kuendelea na elimu ya sekondari, na hapo ndipo alipoanza kujikita kwenye muziki. Mwaka wa 2005 akatoa nyimbo yake ya kwanza "Nakwenda Vikindu". Marafiki na mashabiki wakamshauri kuendelea kwenye muziki.

    Mwaka 2008, alialikwa kufanya onyesho katika tamasha iliyoandaliwa na Times FM ambalo pia ilimjumuisha mwanamuziki Fuse ODG kutoka Ghana. Hii ilimuongezea umaarufu na kujiamini. Mwaka 2009, alifanya kazi pamoja na wasanii wa ndani ikiwa ni pamoja na Alikiba, Yamoto Band, Madee na Snura kwenye kampeni dhidi ya ugonjwa wa Malaria.

    Tangu wakati huo, S Kide ameandika nyimbo 150, ikiwa ni pamoja na "Diamond Kabla Hajatoka" ambayo sasa ina maoni ya nusu milioni kwenye YouTube.