4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: search > Sarabi
Results: 1 to 1 of 1
  • Sarabi

    Country  Kenya
    Genres band urban rock reggae
    Website /pages/SARABI/260804687286737
    FestivalSauti za Busara 2015, 2017
    Recordings📼

    Oyaore (album), 2013 ; Suluhisho (single), 2013; Toto Africa (single), 2013 ; Fuata Sheria (single), 2013

    Sheria by Sarabi Band Feat. Juliani

    Sarabi
    Sarabi

    Gazeti la Buzz liliisifu Sarabi kama“nyuso mpya za muziki wa kisasa wa kiafrika kutoka Kenya”.

    Sarabi iliundwa mwaka 2005, kwa miaka ya karibuni, Sarabi wamekuwa ni wasanii wanaoheshimika kutoka Kenya.  Kikundi hichi kina wasanii wanane wanaotoka sehemu za kimasikinisana huko Kenya.  Walianza kupiga muziki pamoja wakiwa wadogo kama na umri wa miaka kumi na moja tu.

    Muziki wao unatokana muziki wabenga, ukichanganyika na muziki wa Ulaya. Mwaka 2013, alitoa albamu yaoinayoitwa Oyaore.  Mwaka 2014, walitoa albamu yao ya Sheria ambayo ilimjumuisha muimbaji Juliani pia, wimbo huu ulipendwa sana kwa vile ulikuwa unazungumzia kuhusu sakata la mahindi, pia kuhusu kulipia ada za shule, ukosefu wa kazi kwa vijana na jinsi rushwa ilivyotawala kwenye jamii.

    Sarabi ni wanamuziki wachangamfu sana wanapokuwa jukwaani.  Wamewahi kuja kwenye tamasha la Sauti za Busara mwaka 2015, pia walikwenda Ethiopia kwenye tamasha la Selam, na tamasha la Bayimba huko Kampala.  Walishiriki DOADOA na pia kwenye maonyesho mbalimbali huko Dar es Salaam. 

    Mwaka 2015 walifanya maonyesho kadhaa huko bara la Ulaya, walishiriki tamasha la Africa Oye linalofanyika Liverpool nchini Uingereza.  Na walishiriki kwenye tamasha la WOMEX mwaka huo huo.

     

     

    travel-Africalia
    with thanks to Africalia