4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: search > Shirikisho Sanaa Group
Results: 1 to 1 of 1
  • Shirikisho Sanaa Group

    Country  Zanzibar
    Genres traditional roots
    FestivalSauti za Busara 2010, 2012, 2015
    Shirikisho Sanaa Group
    Shirikisho Sanaa Group

    Mwaka 2005 vijana wawili wenye vipaji vya sanaa Mussa Ramadhani na Juma Ally walipata wazo la kuanzisha kikundi ili kujitengenezea ajira. Walitengeneza kikundi cha wanaume 5 na wanawake 3, wakicheza Ngoma mbalimbali zenye asili ya Zanzibar na kusini mwa Tanzania, na hatimaye kundi likakuwa kwa haraka.
    Nguvu, ubunifu na mchanganyiko wa Ngoma mbalimbali ilikuwa ni sababu tosha ya kupata mialiko ya kufanya maonyesho kwenye matamasha na au kwenye hafla nyingine katika maeneo mbalimbali Zanzibar. Maonyesho yao yanajumuisha ngongoti, kuvaa vinyago vya kimakonde, kucheza na moto, na vilevile wanaume na wanawake hucheza Ngoma mbalimbali za mikoa ya kusini mwa Tanzania.
    Miongoni mwa ala za mziki wanazozitumia ni Ngoma, zumari, filimbi, kengele na mapembe.