Results: 1 to 1 of 1
Super Mazembe
Country DRC Kenya Genres band rumba Website www.soundafrica.net Festival Sauti za Busara 2012 Recordings 📼 Giants of East Africa (2001); Greatest Hits Remix (2007)
Utakapotaja bendi ambazo zimehamia afrika mashariki huwezi kuisahau kuitaja Super Mazembe, ambayo imesimama kikamilifu ikiendeleza ushindani katika muziki.
Super Mazembe ilianzishwa mwaka 1969 katika mji wa Likasi karibu na mji wa Lubumbashi, bendi ilihamia Nairobi mwaka 1974, ambapo bendi nyingi kutoka Congo zilikuwepo Tanzania. Walifanikiwa kuteka mashabiki kwa kiasi kikubwa zaidi.
Walibuni aina yao ya uchezaji ijulikanayo kwa jina la mushosho, walizidi umaarufu dhidi ya wapinzani wao Les Mangelepa, Les Kinois, Les Wanyika na Orchestra Virunga. Bendi nyingi zilizuiwa kutokana na mikataba ya kufanya maonyesho ya nyumbani lakini kwa sasa inajulikana kwa jina la Bana Mushosho. Wamezunguka nchi nzima na kufanya maonyesho Uganda na Tanzania, kuwapagawisha mashabiki wao kila waonekanapo.
Mwimbo uliotia fora ni “Shauri yako” na nyimbo zingine ambazo ni maarufu mpaka sasa ni “Samba”, “Bwana Nipie Pesa” na “Kasongo”.
Ilipofika mwaka 1982 bendi ilisimamisha kurekodi lakini ilikuwa inaendelea kufanya maonysho. Kasongo wa kanena alisikika tena mwaka 2006.