4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: search > The Moreira Project
Results: 1 to 1 of 1
  • The Moreira Project

    Country  Mozambique South Africa
    Genres jazz
    Website www.moreiramusic.com
    FestivalSauti za Busara 2009
    Recordings📼

    The Moreira Project Volume 1 - The Journey, 2005; The Moreira Project Volume 2 - Citizen of the World; 2008; Khanimambo: A tribute to the legends of Mozambique, 2011

    The Moreira Project - Ancestrology

    The Moreira Project
    The Moreira Project

    Moreira Changuica mwanamuziki wa Jazz kutoka Mozambique lakini aliyehamia nchini Afrika Kusini ndani ya mji wa Cape Town ambako alikopatia digrii ya muziki mwaka 2000. Moreira ni mtaalam wa muziki wa Jazz kutoka Afrika na dunia kwa ujumla.

    Mwaka 2006 alitoa albam yake aliyeipa jina la “Moreira Project Volume 1” na kufanikiwa kuviteka vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi. Alipotoa albamu yake alichangia pesa kwa ajili ya ukarabati wa shule ya muziki mjini Maputo, shule ambayo alikuwa anasoma alipokuwa mdogo. Muda wowote anapokuwa Maputo atahakikisha anatembelea shuleni kwake kwa ajili ya kukutana na wanafunzi na kuwafundisha kupiga Tarumbeta na kuendesha semina.

    Albamu yake aliitoa mwishoni mwa mwaka 2006, si tu kwamba ilifanikiwa kuingia katika ramani ya muziki lakini ilimtambulisha kuwa kama Msanii, na ikafanikiwa kupata tuzo nchini Afrika Kusini mwaka 2007.

    Albamu yake ya pili aliitoa mwaka 2008 akaipa jina la “Moreira Project Volume 2” bila shaka ilionyesha jinsi gani ametumia kipaji chake na kufanikiwa kunyakua tuzo mbili za SAMA “Muziki bora wa Jazz ya kisasa” na “Albam Bora” mwezi wa tano mwaka 2009.
    Albam yake ya karibuni “Kanimambo” ni mchanganyiko wa sauti za Msumbiji kama Zena Bacar – Nampula, Chico António- Maputo, Chico da Conceiço- Inhambane, Aly Faque- Nampula, Elvira Viegas- Maputo, Júlia Mwito- Capo del Gardo, Wazimbo- Maputo, Xidiminguana na Hortêncio Langa- Gaza,  Dilon Djindje – Marracuene na maelezo na ufafanuzi ukifanywa na Moisés Mandlate – Maputo.

    Moreira alishawasikiliza wanamuziki kwa miaka mingi kupitia kituo chao cha radio cha zamani “LM Radio Station” na kuchukuliwa na baba yake kwa ajili ya kuwaona wakifanya maonyesho yao. Moreira anasema “ kila nilipokuwa nakutana na msanii kila mmoja alikuwa ananiletea nyimbo na nyingine.

    Akasema tena “natumai hii albam itapelekea muziki wa Msumbiji kutambulika kimataifa na kusaidia kuiunganisha nchi. Natumai itaielezea maisha ya watu wa Msumbiji na utofauti wao wa kimaeneo, lugha mbalimbali na nyimba za nchi hii kubwa. Kila msanii aliimba kwa lugha yake na kutoa maoni yake na kuelezea asili ya nyimbo husika. Ilikuwa inauma kutokana na historia na hisia zao lakini kulikuwa na matumaini. Katika albam hii kuna mada zaidi ya 10. Ni utekelezaji na utambuzi wa ndoto na kuwaunganisha marafiki wa zamani.