4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: search > Wamwiduka Band
Results: 1 to 1 of 1
  • Wamwiduka Band

    Country  Tanzania
    Genres roots acoustic
    Website www.wamwiduka.com
    Facebook /Wamwiduka
    FestivalSauti za Busara 2019, 2022
    Recordings📼2019 - Ni Wewe (Single) 2018 - Kilingeni (Single) 2015 - Mama Wema (Single)

    Wamwiduka Band - Wewe zuwena (LIVE @ SAUTI ZA BUSARA)

    Wamwiduka Band
    Wamwiduka Band

     Wamwiduka Band ni wanamuziki ngoma za asili kutoka Mbeya, Tanzania.

    Band ilianziishwa mwaka 2012, ikimjumuisha Brown Isaya (Muimbaji Kiongozi), Adriano Wilson (Mpiga Gitaa na Banjo), Zakaria Michael (Muimbaji na Mpiga ala) and Peter Mashaka (bass na babatoni). Katika kundi hili hakuna hata mwenye elimu ya upili kwahiyo wametumia muda wao katika kujifunza muziki, kuimba na kupiga ala pamoja na kucheza. Muziki ilikuwa ndio njia yao mahsusi ya kujiepusha kutokuchanganyikiwa kwa kutokuwa na ajira.

    Iliwashtua sana walipoanza kupata mialiko ya kufanya maonyesho jukwaani. Muziki wa Wamwiduka Band huchanganywa na gitaa, babatone na sauti za kiasili ambazo hukufanya ufurahi na kucheza.

    Bendi ilifanya onyesho kabambe katika tamasha la Sauti za Busara 2019, kwa sasa bendi imeshajipatia umaarufu ukanda mzima wa Afrika Mashariki na kufanya maonyesho mara kwa mara katika sehemu za kijamii kama vitua vya basi, masokoni na baa.