4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: search > Wamwiduka Band
Results: 1 to 1 of 1
 • Wamwiduka Band

  CountryTanzania
  Genresroots acoustic
  Website

  www.wamwiduka.com

  Facebookwww.facebook.com/Wamwiduka
  FestivalSauti za Busara 2019
  Recordings

   Moyo, 2016; Kilingeni, 2017; Ni Wewe, 2018

  Wamwiduka Band
  Wamwiduka Band

  Wamwiduka Band huchanganya gitaa ya umeme na vionjjo vya asili kwa njia ya ustadi na zenye kusisimua ambazo zikikukuta zitakufanya utabasamu.

  Wamwiduka Band iliundwa miaka sita iliyopita katika mkoa wa Mbeya, ikijumuisha mtunzi, na muimbaji kiongozi, Brown Isaya, Gitaa/ Banjo inapigwa na Adriano Wilson, huku Zakaria Michael kwenye Percussion na kumalizia na Peter Mashaka kwenye Bass/ Babaton.

  Neno Wamwiduka linatokana na lugha ya Safwa, ikiwa na maana ya mwenyeduka. Bendi inapiga Babatoni, ala ya muziki inayopatikana katika Mkoa wa Mbeya lakinni vilevile katika Nchi jirani ya Malawi, ambao nao wanatengeneza ala ya nyuzi nne ili kupata sauti ya Banjo.

   

  Kwa bahati hakuna wanachama wa bendi ya Wamwiduka aliye na elimu ya sekondari hivyo walitumia muda mwingi wao wa kufanya muziki. Muziki ulikuwa kama kiburudisho na kitulizo kutokana na shida za kila siku ikiwemo kukosa kazi. Ilikuja kushangaza Zaidi wakati walipoanza kupata mialiko ya kufanya maonyesho katika sherehe mbalimbali. Sasa bendi ni maarufu kote Dar es Salaam, ambapo hufanya maonyesho mara kwa mara katika maeneo ya umma kama vituo vya basi, masoko na baa.