4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: search > Zee Town Sojaz
Results: 1 to 1 of 1
 • Zee Town Sojaz

  Country  Zanzibar
  Genres hiphop
  Website www.zeetownsojaz.blogspot.com
  FestivalSauti za Busara: 2015

  Chiwile Tv - ZEE TOWN SOJAZ FT RICCO SINGLE - BADO RMX (Officiall Video)

  Zee Town Sojaz
  Zee Town Sojaz

  Zee Town Sojaz ni kikundi cha hiphop kutoka Zanzibar. Kikundi kilianzishwa mwaka 2011 na wasanii mashuhuri wa zenzi flava: King Pozza, Kira Kirami and Chaby Six, baada ya kila mmoja wao kutoa nyimbo zilizopata kupigwa sana kwenye vituo mbalimbali ya redio vya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla. 
  Kila mmoja alitaka kumjua mwenzie kwa bahati nzuri wote walikutana ndani ya studio ya Jupiter Records, Zanzibar, baada ya mazungumzo marefu mwishowe wakakubaliana kuanzisha kikundi. King Pozza alikuja na pendekezo la jina la Zee Town Sojaz.
  Nyimbo yao ya kwanza kama kikundi walimshirikisha Chiku K wa La familia, na kwa bahati nzuri ilipokelewa vizuri. Mwaka 2012 Chaby Six alijitoa kwenye kikundi. Mwaka huohuo alitengea toleo la pili ya nyimbo waliyomshirikisha Chiku K na kutengeneza nyingine wakishirikiana na Dully Sykes “Usiogope” na baadae na Ben Poul “Nakupa Kisogo”
  Kati ya mwaka 2012 mwezi wa sita mpaka mwezi wa tatu 2013 King Pozza alikuwa anamalizia mwaka wake wa  tatu wa elimu yake ya Chuo na Kira Kirami aliendelea na mambo mengine kwahiyo walisimamisha harakati za mziki. Mwezi wa tano 2013 walirudi tena kufanya rekodi ya kibao kipya “Chinjachina”.
  Lengo la Zee Town Sojaz ni kupeperusha bendera ya hiphop ya Zanzibar na kujulikana dunia nzima.