4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
 • Evans 'Pfumela' Mapfumo

  Country  Zimbabwe
  Genres band roots
  Facebook /evansmapfumomusic
  FestivalSauti za Busara 2022

  TORAI NGUVA - Evans 'Pfumela' Mapfumo

  Evans
  Evans 'Pfumela' Mapfumo

  Evans 'Pfumela' Mapfumo ni muimbaji, muandishi na mpiga gitaa kutoka Zimbabwe. Muziki wake umebeba ujumbe maridhawa kuhusu vita, umasikini, utesaji wa watoto pamoja na kuhamasisha Amani, upendo na mshikamano.

  Bendi yake inafanya maonyesho kabambe yenye kuchanganya mashairi ya utamaduni, marimba na mbira, gita na vifaaa vingine vya kitamaduni. Wamashafanya maonyesho kwenye matamasha mbalimbali ikiwemo World Cup Fan Festival in South Africa (2010), Cape Town Summer Market Festival (2012), National Arts Festival (South Africa) na Harare International Festival of the Arts (HIFA, 2015).

  Evans Mapfumo ana shahada Muziki na sasa ni mhadhiri wa chuo cha muziki, Zimbabwe College of Music.