4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
 • Sona Jobarteh

  Country  Gambia UK
  Genres roots traditional
  Website www.sonajobarteh.com
  FestivalSauti za Busara 2014
  Recordings

  Fasiya, 2011

  Sona Jobarteh
  Sona Jobarteh

  Sona Jobarteh ni msichana wa kwanza kupiga Kora na vifaa mbalimbali vya muziki, Kuimba, kutunga nyimbo kutoka katika familia ya Griot. Alizaliwa mwaka 1983 nchini Gambia (Afrika ya Magharibi). Sona ametokea katika familia ya wanamuziki, Mjukuu wa Amadu Bansang Jobarteh, binamu wa mpiga Kora maarufu Toumani Diabate na vile vile dada wa Tunde Jegede. Alianza kujifunza kupiga kora tangu alipokuwa na umri wa miaka mitatu na kufanya onyesho lake la kwanza akiwa na umri wa miaka minne katika mkahawa wa London Jazz Café. Amejifunza mambo mbalimbali katika chuo cha muziki cha "Royal College" ikiwemo Piano na harpsichord na baadae amekwenda chuo cha Purcell kwa ajili ya kujifunza utunzi wa muziki. Katika kipindi hicho alijihusisha na miradi kadhaa ya kimuziki kama "River of Sound" akishirikiana na Irish Chamber Orchestral na kufanya maonyesho ya pamoja na Royal Philharmonic Orchestra, Britten Sinfonia, Milton Keynes City Orchestra na Viva Chamber Orchestra. Mbali na hayo ameshikiriana na wasanii kutoka sehemu mbalibmali duniani, ni mmoja kati ya wanachama wa African Classical Music Ensemble ambayo imeshawahi kufanya ziara za kimuziki sehemu mbalimbali duniani ikiwemo Uingereza, Ireland, Visiwa vya Karibian na Afrika. Jobarteh hutumia muda wake kufanya maonyesho na kutoa elimu ya upigaji wa Kora kwa ajili ya kuendelea utamaduni wa upigaji wa Kora kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

  ACE_BritishCouncil_White_RGB
  With thanks to the Arts Council England and the British Council