Hoko Roro
Country Tanzania Genres acoustic fusion Festival Sauti za Busara 2014 Kundi la Hoko Roro limeanzishwa na kijana mwenye kipaji ajulikanaye Samuel Hoko Roro ambaye alizaliwa mwaka 1990 katika Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam. Samuel alianza kuimba alipokuwa na umri wa miaka minane, alikuwa anaimba Nyumbani, Shule na Kanisani.
Samuel alikuwa anajiuliza mwenyewe ni lini ndoto yake ya kumiliki bendi itatimia. Mwaka 2006 alikwenda kwenye kituo cha kulelea watoto wa mitaani cha “Dogodogo Center” alifanikiwa kupata mafunzo ya muziki ikiwemo kucheza na kupiga vifaa vya muziki. Hapo ndipo alipopata nafasi ya kujifunza kupiga Gitaa. Kwa kuwa Samuel alikuwa makini darasani aliweza kufanya vizuri kwenye masomo yake na tangu alipomaliza masomo yake mwaka 2008 aliendelea na masuala ya muziki kwa muda wote.
Mwaka 2011 nyota yake ilianza kun’gaa alichaguliwa kushiriki kwa mara kwanza kwenye tamasha la “Visa2Dance” na mwaka huo huo alipata safari ya kimuziki nchini Unganda na Ujerumani na kundi la Lumumba theatre nako alipata mafunzo zaidi.
IMwaka 2012 alijaribu kutaka kujiendeleza kwenye fani yake ya muziki alikwenda kwenye chuo cha muziki Zanzibar “Dhow Country Music Academy” (DCMA) lakini alishindwa kuendelea na masomo kutokana na ukata wa ada ndipo alipoamua kurudi Dar es Salaam kuendelea na masuala yake ya muziki kama kawaida.
Mwaka 2013 ndoto ilitimia kwa kuanzisha bendi yake ijulikanayo Hoko Roro pamoja na wasanii wenzake kama Mohammed Twaba, Ilali Mohammed na yeye mwenyewe.
Algeria Angola Australia Austria Benin Burkina Faso Burundi Cameroon Canada Cape Verde Comoros Congo Côte d'Ivoire Denmark DRC Egypt eSwatini Ethiopia Far East Finland France Gambia Germany Ghana Guinea Guinea Bissau Iraq Japan Kenya Lesotho Madagascar Malawi Mali Mauritania Mauritius Mayotte Morocco Mozambique Namibia Netherlands Nigeria Norway Pan Africa Pemba Puerto Rico Reunion Rwanda Senegal Seychelles Somaliland South Africa Sudan Suriname Sweden Switzerland Tanzania Uganda UK USA Various Yemen Zambia Zanzibar Zimbabwe
acoustic acrobats afrobeat band blues bongo flava coastal comedy dance dj electro fusion hiphop jazz kidumbak pop reggae rock roots rumba spiritual spoken word taarab traditional urban zenji flava