4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
  • Matona's G Clef Band

    Country  Zanzibar
    Genres fusion
    Website /mohamed.matona
    FestivalSauti za Busara 2017
    Recordings📼

    Urithi 2006

    Matona Swahili Jazz

    Matona
    Matona's G Clef Band

    Kikundi cha G Clef au kwa jina jengine kinajulikana kama ‘Kikundi cha Matona’, kilianzishwa mwaka 1995 baada ya kubinafsishwa kwa hoteli ya Bwawani.  Matona alikuwa kiongozi wa kikundi kilichojulikana kama Kikundi cha Taarab cha Bwawani, hoteli ilipobinafsishwa kikundi hakikuvunjika, kiliendelea kwa jina jengine ambalo ni G Clef Taarab Orchestra, wanakikundi hawa waliendeleza kupiga muziki wa taarab.Na pale wanamuziki wakongwe walipokuwa wakihama kikundi, Matona alikuwa akileta wanamuziki vijana ambao akiwafundisha ujuzi mwenyewe.Hatimaye kikundi hichi kikawa maarufu Zanzibar. Wakawa manapiga nyimbo tofauti, hata za kihindi, kiarabu, muziki wa dansi na hata muziki wa rock.

    Kikundi hichi kilisitisha sanaa kwa muda pale Matona alipojishughulisha na ufunguzi wa shule ya muziki ya DCMA mwaka 2001.  Matona alikifufua kikundi hichi mwaka 2015 baada ya kuona kuna nafasi ya kuwepo kikundi cha muziki ambacho kitapiga aina tofauti za muziki.  Na sasa ni kikundi kinachojulikana sana mjini.  Madhumuni yao ni kuendeleza aina tofauti za miziki inayopigwa katika nchi za afrika ya mashariki kama vile taarab, mgodro, salege, chakacha, sega, na mbiwi.