4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
  • Zenji Boy na Wenzake

    Country  Zanzibar
    Genres hiphop fusion zenji flava
    Website www.musicinafrica.net
    Facebook /OfficialZenjiboy
    FestivalSauti za Busara 2020, 2021, 2023
    Recordings📼Nani Niliomkosea, 2017; Sina Hakika na Kesho, 2018; Monster, 2018; No Place Like Home, 2018; My Talent, 2018; Mazabe, 2019; Zenji Boy, 2019

    Zenji Boy na Wenzake
    Zenji Boy na Wenzake

    Zenji Boy (Ison Mistari) ndiye rapper, dj na mtayarishaji maarufu zaidi Zanzibar. Muziki wake umechangiwa na mitindo ya muziki wa kiasili ikiwa ni pamoja na taarab, kidumbak na msewe (ngoma kutoka kisiwa cha Pemba), ambayo anaichanganya kwa ufasaha na hiphop.

    Uandishi wa nyimbo wa Zenji Boy ni muhimu na makini, wenye ujumbe mzito ambao unahusu hadhira yake inayozungumza Kiswahili. Nyimbo zake zinazungumzia siasa, upendo, umoja, jamii na maendeleo ya kijamii. Maonyesho yake ya moja kwa moja yana vutia sana. Amepata heshima na kuthaminiwa nyumbani na nje ya nchi kwakuitumia kwa ustadi violin na oud katika mitiririko yake ya sauti.

    Zenji Boy alishinda Video Bora ya Muziki 2017 na Kitendo Bora cha Kiume 2018 kwenye Tuzo za Zenj255, Tuzo ya Emerson Foundation 2020 na Msanii Bora wa Mwaka 2021 katika Tuzo za Vijana Zanzibar.