4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
  • Seven Survivor

    Country  Tanzania
    Genres coastal roots urban
    FestivalSauti za Busara 2008, 2012, 2014
    Recordings📼

    Panya wa Dar es Salaam, 2007
    Kilio cha Mastaa, 2013
     

    Seven Survivor
    Seven Survivor

    Kikundi hichi kilianza rasmi mwaka 1995 kilijulikana kwa jina la Survival Original lakini baada ya miaka baadaye kutokana na kutokuelewana, baadhi ya memba walisababisha kuanzishwa rasmi kundi la Seven Survivor.Seven Survivor ni kikundi kimoja wapo ambacho kinaongoza katika muziki wa mchiriku ndani ya jiji la Dar es Salaam. Aina hii ya muziki ambayo ni maarufu sana katika mji wa Dar es Salaam, mkoa wa pwani na Morogoro. Mchiriku imepigiwa kwa zaidi ya miaka ishirini sasa hasa kwenye sehemu ya watu wenye kipato cha chini.Kundi limeshafanikiwa kutoa albam 18 za kaseti na albam ya mwisho waliitoa mwaka 2007 yenye jina la Panya wa Dar es salaam.Mwanzoni mwa mwaka 2012 Juma Mpogo alifariki dunia kipindi ambacho kilikuwa karibu na Tamasha la Sauti za Busara lakini kundi liliweza kukonga nyoyo za mashabiki wao.Mwaka uliofuata 2013 wametoa albam yao mpya waliyoipa jina la "kilio cha mastaa" ikiwani kumbukumbu ya kumkumbuka kiongozi wao (Juma Mpogo) na wasanii wengine walioiaga dunia.Kiongozi wa kundi hilo Juma Mpogo anasema wanalazimika kutoa albamu nyingi kwa sababu wanaondelesha soko la muziki huo hawawalipi vizuri. Hawana meneja mwenye utaalamu wala mtu wa kuwasaidia ili waweze kupata shoo mbali mbali.Wanatunga nyimbo mbalimbali zenye historia ya matukio ya kila siku yanayozunguka jamii zao na nchi kwa ujumla. Nyimbo zao nyingi zinaelezea kuhusu matukio ya wizi, madawa ya kulevya, umalaya, ushirikina, ufanyishwaji wa kazi kwa watoto wa chini ya umri wa miaka 18 na migogogro tofauti.Usikose kuwaona tena na mwimbaji wao mpya Hamad Kihedu (ndugu wa Juma Mpogo) wakipanda juu ya jukwaa la tamasha la Sauti za Busara 2014.