4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
 • African Stars Band (aka Twanga Pepeta)

  Country  Tanzania
  Genres band dance rumba
  Website www.africanstars.net
  FestivalSauti za Busara 2011
  Recordings

  Kisa cha Mpemba (1999) Jirani (2000) Fainalu Uzeeni (2001) Chuki Binafsi (2002) Ukubwa Jiwe (2003) Mtu Pesa (2004) Safari (2005)

  African Stars Band (aka Twanga Pepeta)
  African Stars Band (aka Twanga Pepeta)

  Ni miongoni mwa bendi liiyo na wapenzi wengi sana,inatambulika Tanzania kama Twanga pepeta kutokana na mtindo wake wa kiuchezaji. Wameshafanikiwa kupata tunzo nyingi tangu ilipoanzishwa mnamo mwaka 1994. Ilishapata tuzo ya kuwa bendi bora ya mwaka, tuzo ya uchezaji bora na bendi bora ya mziki wa dance na wameshafanikiwa kutoa santuri nane zikiwemo za kusikiliza na kuona na nyimbo nyingi kati ya hizo zimefanikiwa sana mpaka kupata tuzo za mwimbo bora, kama mwimbo wa Mtu Pesa. Bendi inachanganya mitindo tofauti kama Rhumba, Ndombolo, Blues, Chacha, Zouk na hata Soca. Katika tamasha la mwaka 2011 la Sauti za Busara Twanga Pepeta watapandisha stejini watu 17 kati ya 40 ambao ni wanachama wa kundi. Bendi nzima itashusha burudani na kutoa show ya kukata na shoka siku ya mwisho ya kufunga tamasha.