4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
  • Hanitra

    Country  Madagascar
    Genres acoustic
    Website www.hanitra.com
    FestivalSauti za Busara 2012
    Recordings📼

    Any Aminay (2010)

    IOMMA 2011 - Premier marché des Musiques de l'Océan Indien

    Hanitra
    Hanitra

    Hanitra ni mwimbaji na mpiga gitaa kutoka kisiwa cha Madagascar.  Misingi ya nyimbo zake unatokana na haiba ya muziki ya Madagascar, pamoja na vionjo kutoka Cuba na Brazil, alichukua nyimbo za asili kwa nguvu na hatimaye kuwakilisha kizazi cha Malagasi. Sauti ya kuvutia ndio iliyomfanya kuwa mmoja kati ya wasanii ambao uchukuliwa kama mwimbo wa taifa wa Madagascar.

    Hanitra alianza kuimba na kupiga gitaa alipokuwa na umri wa miaka saba. Mwaka 1979, alishiriki katika shindano la kitaifa ambapo kipaji chake kiligunduliwa rasmi na kujiunga na bendi moja kwa moja ya Lolo Sy Ny Tariny. Alienda Ufaransa akitokea Madagascar. Mwaka 1997 alirudi Madagascar. Kwa sasa anaishi katika kisiwa cha Reunion na ana shauku kubwa ya kuburudika na mashabiki wake wote katika ukanda wa Bahari ya Hindi.