Wanafunzi wa SOS
Country Zanzibar Genres roots traditional Festival Sauti za Busara 2012, 2013 Huu ni mseto wa watoto yatima ambao wapo chini ya skuli ya Hermann Gmeiner iliyopo Zanzibar katika kijiji cha kulelea watoto yatima cha SOS.
Watoto waliopoteza wazazi wao huchikuliwa na katika harakati za kuwapa malezi bora, elimu, afya na mafunzo jinsi ya kuishi na jamii tofauti ndani na nje ya zanzibar. Vili vile shule ina mpango madhubuti wa kuvilea vipaji vya watoto kwa kuwataka wawe huru kuchagua mchezo wanaoutaka.
Shule ilianzisha darasa maalumu kwa ajili ya ngoma za utamaduni kutoka zanzibar na Tanzania ili kuviendeleza vipaji vyao.
Mwaka 1991 kikundi kilianzishwa rasmi na vijana wapatao 18 wote wanafunzi wa SOS baada ya kuwa na kazi kubwa ya kuwachagua na baadae kufanikiwa kuwapata wakali zaidi na wanaendelea kutoa burudani ya nguvu ndani na nje ya zanzibar.
Hucheza msewe ngoma ambayo maarufu Zanzibar kutoka katika kisiwa cha Pemba ambayo huchezwa katika sherehe mbali mbali kama kwenye harusi, mavuno na sherehe za serikali.
Kama nilivyosema awali kikundi hiki ni mseto wa vipaji kwa kuthibitisha hili wameweza kutumia vifaa mbali mbali vya muziki kama ngoma mbalimbali, filimbi, masewe, manyanga na aina nyingine katika maonyesho yao.
Katika ujumbe wao hupendelea kuiasa dunia kulisa usalama na amani kwa kuwa kupindi cha vita vya wenyewe kwa wenyewe watu ambao wenye hatari ya kupoteza maisha ni akina mama na watoto.
Algeria Angola Australia Austria Benin Burkina Faso Burundi Cameroon Canada Cape Verde Comoros Congo Côte d'Ivoire Denmark DRC Egypt eSwatini Ethiopia Far East Finland France Gambia Germany Ghana Guinea Guinea Bissau Iraq Japan Kenya Lesotho Madagascar Malawi Mali Mauritania Mauritius Mayotte Morocco Mozambique Namibia Netherlands Nigeria Norway Pan Africa Pemba Puerto Rico Reunion Rwanda Senegal Seychelles Somaliland South Africa Sudan Suriname Sweden Switzerland Tanzania Uganda UK USA Various Yemen Zambia Zanzibar Zimbabwe
acoustic acrobats afrobeat band blues bongo flava coastal comedy dance dj electro fusion hiphop jazz kidumbak pop reggae rock roots rumba spiritual spoken word taarab traditional urban zenji flava