4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
  • Atongo Zimba

    Country  Ghana UK
    Genres acoustic roots
    Website www.atongozimba.com
    Facebook /AtongoZimbaOfficial
    Instagram /atongo.zimba
    FestivalSauti za Busara 2006, 2013
    Recordings📼

    Allah Mungode, 1994; MC Combination, 1996; Savannah Breeze, (Hippo Records 2005); Barefoot In the Sand, 2007; Sakune Music, 2009

    Atongo Zimba in front of 40.000 spectators in Amsterdam

    Atongo Zimba
    Atongo Zimba

    Atongo Zimba, mwanamuziki kutoka Ghana. Safari ya usanii ilianzia kutoka kwa Babu yake ambaye alimfundisha kutengeneza na kutumia Koliko (molo) kifaa ambacho ni maarufu katika maeneo ya Savannah na katika ukanda wa jangwa la Afrika Magharibi.

    Kipindi cha sikukuu na mwisho wa wiki alikuwa anautumia kwenda kutafuta malisho kwa ajili ya mifugo yao. Kulikuwa na tamaduni tofauti kutoka kwa baadhi ya wafugaji ambao wengi wao waliweza kupiga vifaa tofauti vya muziki na kufanya vionjo vya sauti, kuiga sauti za ndege na wanyama.

    Alijifunza nyimbo za kitamaduni na kuanza kutunga za kwake kwa kutumia Koliko na kupiga nyimbo mbalimbali. Koliko hutumika katika shughuli mbalimbali za kijadi na kuwahamasisha Wakulima, lakini Atongo alipendelea kuutambulisha muziki kuwa ni kazi, alifanya ziara yake mpaka Nigeria katika kiwanja cha Fela Kuti ambaye alikaa kwa miaka miwili kipindi cha ujana wake, alifanya maonyesho ya mwisho wa wiki peke yake (Solo)

    Alirudi Ghana katika kipindi cha miaka ya 80 na 90 akapiga na Osibisa na Pan Afrika Orchestra. Katika kipindi hicho hicho alifanikiwa kuboresha aina yake ya upigaji wa peke yake, kuchukua vionjo vya "jazz" na "funk".

    Atongo aliimba nyimbo zenye asili ya Lugha ya Fra Fra, Hausa, Ga, Kingereza na Twi. Maudhui ya nyimbo zake yaliangazia katika nyanja mbalimbali kama Mamlaka, heshima katika mahusiano ya kikabila, masuala ya maisha ya kila siku, maendeleo ya Ghana na Afrika kwa ujumla na watu kupendana.

    Atongo ameshatoa albam nne nchini Ghana. Tangu mwaka 2003 alihamishia makazi yake nchini Uingereza, pamoja na kuwa ni kiunganishi madhubuti kwa wanamuziki wa nchini mwake. Alishafanya maonyesho katika matamasha mbalimbali ndani ya Ulaya, Afrika na Latin Amerika.

     

    GI_Logo_horizontal_green
    With thanks to Goethe Institut