Mashauzi Classic Modern Taarab
Country Tanzania Genres band coastal pop Festival Sauti za Busara 2012 kundi la mashauzi classic ni moja kati ya makundi maarufu Tanzania bara na visiwani katika tasnia ya muziki wa taarabu ya kisasa (Modern Taarab)
Ilianza kupata umaarufu katika miaka ya 1990, kilikuwa kilio cha muda mrefu kutoka kwa wanamuziki wa zamani wanaopiga taarab asilia na wakilalimika kwamba hii sio taarab. Lakini bado iliendelea kupata umaarufu na kupendwa hasa na wanawake kutokana na ujumbe na midundo yake inayohamasisha kucheza.
Mashauzi Classic Modern Taarab ilianzishwa mwaka 2011 na wanamuziki maarufu wawili, Isha Ramadhan na Thabit Abdul ambao walifanikiwa kuvuta hisia za mashabiki wao kwa haraka kutokana na mfumo wa uimbaji na uchezaji.
Isha Ramadhan maarufu Isha mashauzi, safari yake ya muziki amepitia vikundi tofauti ikiwemo Segere Original. Aalijiunga na Jahazi Modern Taarab mwaka 2007 kutokana na ushauri wa mzee Juma Mbizo, alianza kutambulika katika tasnia ya taarab ya kisasa alipoimba mwimbo wa kwanza “Hayanifiki” na “Yawenzenu Midomoni”. Mwaka 2010 alofanikiwa kutoa albamu yake mwenyewe aliyoipa jina “Mama nipe radhi” katika mwaka huo Thabit Abdul alijiunga na Jahazi Modern Taarab na ndipo walianza matayarisho ya uzinduzi wa kundi lao, ambalo kwa sasa linajulikana kama Mashauzi Classic. Thabit Abdul ni mpaga kinanda maarufu Tanzania na amepitia bendi tofauti ikiwemo Extra Bongo, All Star Modern Taarab, TOT, Jahazi Modern Taarab na African Stars Band (Twanga Pepeta).
Algeria Angola Australia Austria Benin Burkina Faso Burundi Cameroon Canada Cape Verde Comoros Congo Côte d'Ivoire Denmark DRC Egypt eSwatini Ethiopia Far East Finland France Gambia Germany Ghana Guinea Guinea Bissau Iraq Japan Kenya Lesotho Madagascar Malawi Mali Mauritania Mauritius Mayotte Morocco Mozambique Namibia Netherlands Nigeria Norway Pan Africa Pemba Puerto Rico Reunion Rwanda Senegal Seychelles Somaliland South Africa Sudan Suriname Sweden Switzerland Tanzania Uganda UK USA Various Yemen Zambia Zanzibar Zimbabwe
acoustic acrobats afrobeat band blues bongo flava coastal comedy dance dj electro fusion hiphop jazz kidumbak pop reggae rock roots rumba spiritual spoken word taarab traditional urban zenji flava