4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
  • Mokoomba

    Country  Zimbabwe
    Genres band roots fusion
    Website mokoomba.band
    Facebook /mokoomba
    FestivalSauti za Busara 2013, 2019
    Recordings📼

    Kweseka, 2009;  Umvundla EP in collaboration with DJ Gregor Salto, 2011; Rising Tide, 2012;  Luyando, 2017

    Mokoomba - Masangango (Zimbabwe)

    Mokoomba
    Mokoomba

     

    Mokoomba ni bendi inayotoka katika Mji wa Victoria Falls nchini Zimbabwe, mji ambao yanapatikana maporomoko ya maji ambayo ni kati ya maajabu saba ya dunia. Bendi inaundwa na vijana sita ambao wamekuwa pamoja kama marafiki katika kitongoji cha Chinotimba sehemu ambayo walianza kufanya muziki baada ya shule. Katika kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa vifaa walikuwa wanapiga katika shughuli ndogondogo. Bendi inapatikana mpakani mwa Zambia, Namibia na Botswana sehemu ambayo ni kitovu cha utalii, hivyo basi uwepo wa watalii uliwaongezea muonekano wa kimataifa na kuwatofautisha na tasnia ya muziki wa Zimbabwe.

     

    Wanapendwa hasa kutokana na aina ya muziki wao, mashairi na stori mbalimbali zihusuzo asili yao, lugha hasa Luvale, Tonga na Nyanja bila ya kusahau Shona na Ndebele, vilevile wakienda sambamba na midundo ya Soukous kwenda Ska, Funk kwenda Afro-latin wakitoa midundo adimu ya Afrosoul.

     

    Moja ya mafanikio yao makubwa yalikuwa mwaka 2008 waliposhinda mashindano ya Music Crossroads Inter-Regional Festival nchini Malawi, walirekodi albamu (demo) waliyoipa jina la Kweseka na kufanikiwa kufanya ziara ya kimuziki katika bara la ulaya mwaka 2009 na 2010. Mwaka 2011 wakiendelea kuwa na sura ya kimataifa sasa wakatoa albamu yao ya kwanza yenye hadhi ya kimataifa waliyoipa jina la ‘Rising Tide’ chini ya mtayarishaji nguli Manou Gallo chini ya lebo ya ZigZag World, ubelgiji. Albamu ilipokelewa vizuri sana na wadau mbalimbali wa tasnia ya muziki na majarida tofauti ikiwemo Songline Magazine, fRoots Magazine, Afropop Worldwide, NPR na The Guardian ambapo waliorodhesha Rising Tide kama albamu bora 5 bora kwa mwaka 2012.

    Safari ya mafanikio iliendelea kuangazia upande wao ambapo walifanikiwa kupata ziara ya kimuziki takriban nchi 50 dunia nzima kuanzia mwaka 2012 mpaka 2018.

     

    Maonyesho yaliyotia fora ni ya tamasha la Roskilde, Denmark, WOMAD, Uingereza, Australia na New Zealand, WOMEX huko Thessaloniki, Montreal Jazz, Canada, Sziget, Hungaria, Paleo, Uswisi, Pole Pole Festival, Ubelgiji, Gnawa, Morocco, Colors of Ostrava Jamhuri ya Czech, Voice of Nomads, Urusi, New Orleans Jazz & Heritage, Marekani, Gwanju World Music Festival, Korea Kusini, Sauti za Busara Festival, Zanzibar, Afrika Oye, Liverpool, UK na kuonekana kwenye programu ya BBC 2 na Jools Holland. "

     

    Mwaka 2017, Mokoomba walitoa albamu yao mpya ‘Luyando’ nayo ilisifiwa na wapenda muziki, pia alikiri sana na wapenzi wa muziki na lawama. Mwaka 2018, Mokoomba alifanikiwa kuonyeshwa walichaguliwa kwa tuzo ya Songline Music katika kipengele cha kikundi bora. Bendi inaendelea kufanya ziara ndani na nje ya nchi.

    Mokoomba_travel-sponsor-logo_NGOMA-NEHOSHO_croped
    With thanks to NGOMA NEHOSHO