4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
  • Peter Msechu

    Country  Tanzania
    Genres band rumba bongo flava pop
    FestivalSauti za Busara 2013

    Hasira Hasara - Peter Msechu ( Official Video )

    Peter Msechu
    Peter Msechu

    Peter Msechu alizaliwa kaskazini mwa Tanzania katika mkoa wa Kigoma karibu na mpaka wa Tanzania na Burundi. Alianza kuimba alipofikia umri wa miaka kumi ambapo baba yake alimchukuwa kwenda kujiunga na kikundi cha kwaya kanisani, wakati huo baba yake alikuwa mwalimu wa kwaya.

    Mama yake alikuwa Mwalimu wa Shule ya Msingi Katubuka, Mama yake alipenda sana Msechu asome lakini baba yake alitaka Msechu awe Mwanamuziki.

    Mwaka 2009 ndipo alipoanza kutambulika kupitia mashindano ya vipaji yajulikanayo kama “Bongo Star Search (BSS)” yanayoonyeshwa katika kituo cha Televisheni kila wiki. Kipindi cha mashindano alipitia changamoto nyingi kwa kuwa alikuwa amezoea kuimba nyimbo za kwaya wakati washindani wenzake wanaimba nyimbo mbalimbali.

    Alianza kutunga nyimbo zake mwenyewe na alipata msukumo kutoka kwa majaji akina Madam Rita, Salama Jabir, P Funk na Master J ambao walimpa moya sana kipindi cha mashindano. Alibadilisha mbinu za uimbaji na akaanza kuimba nyimbo za zamani na kufanya maonyesho ya kuvutia. Alifanikiwa kuwateka vijana wengi wa Tanzania ambao walikuwa na shauku ya kutaka kuona nini Msechu atawaletea.

    Siku ya mwisho Msechu akawa mshindi wa pili, kwa kuwa ndoto zake zilikuwa kuanzisha bendi, akasema “Muda umewadia” baada ya miezi kadhaa akafanikiwa kutoa nyimbo ya kwanza aliyoipa jina la “Hasira Hasara” ikafuatiwa na nyimbo aliyoshirikiana na Msanii Kidum kutoka Burundi iliyokwenda kwa jina la “Relax”

    Baada ya kupata umaarufu Tanzania nzima, mwaka 2010 alipata nafasi ya kujiunga na mashindano ya “Tusker Project Fame” ni sawa na (BSS) lakini tofauti ni kwamba washiriki wake walikuwa wanatoka nchi

    Aliendelea na ubunifu wake kwa kuimba nyimbo mbalimbali kama za akina Oliver Mtukudzi, Marijani Rajab na Mbaraka Mwinshehe kwa kuchanganya na midundo tofauti. Kwa mara nyingine tena anafanikiwa kuwa mshindi wa pili, na kufanikiwa kumpatia umaarufu na kujiamini zaidi na kuamua kufanya muziki ni kazi.

    Tangu hapo ameshanikiwa kufanya maonyeshi Afrika Mashariki na hivi karibuni ametoka katika ziara ya kimuziki nchini Marekani.