Fadhilee Itulya
Country Kenya Genres roots fusion jazz traditional Website www.presskit.to Facebook /fadhileemusic Festival Sauti za Busara 2019 Recordings 📼 Kwetu, 2018
Fadhilee ni msanii kutoka lakini mwenye maono ya mbali kimuziki. Fadhilee hushirikiana na wasanii mbalimbali kubuni na kutunga nyimbo kwa ajili ya maendeleo ya Sanaa ya Afrika Mashariki. Muziki wake unavutia hasa katika upigaji wa Gitaa akitumia kidole gumba maarufu omutibu. Aina hii ya upigaji inapendwa sana katika maeneo ya magharibi ya Kenya, Kakamega ambapo ni asili ya Baba yake. Mwaka 2018 alitoa albamu yenye nyimbo 10 iliyoenda kwa jina ‘Kwetu’ (Home) albamu ilisheheni nyimbo kali We Don't Know, Kwetu, Shombo, Mama na Flora. Albamu iliwekwa vionjo vya asili vya Luyha Isukuti hivyo iliongeza chachu ya usikilizwaji.
Mpaka sasa Fadhilee ameshafanya maonyesho sehemu mbali ndani ya Afrika Mashariki na nje yake ikiwemo Ghana, Scandinavia, Ujerumani, Ugiriki na Uswizi, mbali na hayo vilevile ni miongoni mwa waanzilishi wa Utam Festival, na Fadhilee’s Garage- shoo ya kila mwezi.With thanks to Africalia
Algeria Angola Australia Austria Benin Burkina Faso Burundi Cameroon Canada Cape Verde Comoros Congo Côte d'Ivoire Denmark DRC Egypt eSwatini Ethiopia Far East Finland France Gambia Germany Ghana Guinea Guinea Bissau Iraq Japan Kenya Lesotho Madagascar Malawi Mali Mauritania Mauritius Mayotte Morocco Mozambique Namibia Netherlands Nigeria Norway Pan Africa Pemba Puerto Rico Reunion Rwanda Senegal Seychelles Somaliland South Africa Sudan Suriname Sweden Switzerland Tanzania Uganda UK USA Various Yemen Zambia Zanzibar Zimbabwe
acoustic acrobats afrobeat band blues bongo flava coastal comedy dance dj electro fusion hiphop jazz kidumbak pop reggae rock roots rumba spiritual spoken word taarab traditional urban zenji flava