4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: By Country > Angola
Results: 2 to 2 of 2
 • Waldemar Bastos

  Country  Angola Portugal
  Genres roots acoustic
  Website www.waldemarbastos.com
  FestivalSauti za Busara 2014
  Recordings

  Moyo" - Keiko Matsui, Shout Factory, 2007, In the Name of Love - Africa Celebrates U2" , Shout Factory 2008

  Waldemar Bastos - Velha Chica

  Waldemar Bastos
  Waldemar Bastos

  Waldemar Bastos alizaliwa mwaka 1954 katika mji wa Zaire ambao ulikuwa mji mkuu wa Angola kipindi cha ukoloni. Wazazi wake wote walikuwa wauguzi wa afya (nurse). Alianza kuimba alipokuwana umri mdogo kabisa.
   “Nilipokuwa mdogo mama yangu aligundua kuwa nina kipaji cha muziki. Nilitumia muda mwingi kuimba na kupiga filimbi ambapo mama yangu aligundua kwamba nina kitu cha ziada naye akaamua kunisaidi”
  Siku moja baba yangu alifika nyumbani akanikuta napiga kifaa chake cha muziki (concertina) ambapo alikihifadhi vizuri katika kabati. Nilijihisi vibaya kuchukua kitu bila ya ridhaa yake na hasa kitu chenyewe anakithamini sana. Lakini bila ya kutegemea alifurahia na ndhani aliridhika zaidi alipokuwa ananisikia kwenye Redio mbalimbali. Na hatimaye kunipa zawadi ya Kinanda (Accordion) siku ya krismas
  Kutoka hapo Waldemar alijikita zaidi kifikra katika muziki, alipokuwa na umri wa miaka nane alisikia matangazo kwenye kituo cha Redio kwamba kuna mwalimu anafundisha muziki. Waldemar aliwaambia wazazi wake na kwa bahati nzuri walikubali. Ingawa kulikuwa na tatizo la kipato lakini haikuwa tatizo kwake ambapo aliwaambia wazazi wake wamnunulie Baiskeli ili iwe rahisi kupata mafunzo.
  Mwaka 1982 alihamia Brazili ambapo mambo yalimwendea vizuri na kupata kuelewa maana ya umoja na mshikamano, aliweza kutoka na albam yake ya kwanza mwaka 1983 aliyoipa jina la “Estamos Junto”
  Mwaka 1985 alihamia Ureno na kufanikiwa kurekodi albamu yake ya pili mwaka 1989 iliyokwenda na jina “Angola Minha Namorada” miezi mitano baadae, mwaka ule ule alikwenda Angola na kufanya onyesho la kihistoria ambalo lilihudhuriwa na watu wasiopungua 200,000 wakifurahia onyesho hilo kwa kupeperusha vitambaa vyeupe. Mambo yaliendelea kumnyookea ambapo mwaka 1992 alikuja tena na albamu yake ya tatu kwa jina la Pitanga Madura (EMI Portugal, 1992)
  Mwaka 1997 akaja na Pretaluz [blacklight] (Luaka Bop, 1997) ikiwa albamu yake ya nne. Na mwaka 2004 “Renascence” na lbamu yake ya sasa ni “Love Is Blindness” aliyoitoa mwaka 2008.

  Tangu alipotoa albamu yake ya tatu ambayo ilipata mafanikio katika Nyanja za vyombo vya habari. Jarida la New York Time lilielezea albamu yake kuwa ni bora na kushinda tuzo ya msanii bora anayechipukia mwaka 1999.

  Estamos Juntos (EMI Records Ltd., 1983)
  Angola Minha Namorada (EMI Portugal, 1989)
  Pitanga Madura (EMI Portugal, 1992)
  Pretaluz [blacklight] (Luaka Bop, 1997)
  Renascence (World Connection, 2004)
  Love Is Blindness (2008)