4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: By Country > Cape Verde
Results: 2 to 2 of 2
 • Tcheka

  Country  Cape Verde
  Genres roots
  Website /tcheka.cv
  FestivalSauti za Busara 2015
  Recordings

  Dor De Mar (2011); Lonji (2007); Nu Monda (2005); Argui! (2002)

  TCHEKA - Agonia

  Tcheka
  Tcheka

  Tcheka alizaliwa na jina la Manuel Lopes Andrade mwaka 1973 eneo la Ribeira da Barca, sehemu ndogo ya kijijini katika pwani ya kijiji cha Santiago, Cape Verde ambayo uchumi wa eneo hilo unategemea kilimo na uvuvi. Alikua mtoto wa pili kutoka mwisho katika familia kubwa yenye historia ya kimuziki. Baba yake, Nho Raul Andrade alikua mpiga zeze maarufu katika eneo lao ambapo alifundisha wanawe wa kiume muziki na baadaye kuunda bendi ya familia ambayo ilikua ikitumbuiza katika sherehe ndogo ndogo kama harusi, mazishi na ubatizo. Tcheka anasema alijifunza kupiga gitaa kwa lazima akiwa na umri wa miaka 8 na alipofikisha miaka 9 aliweza kutumbuiza kucheza na bendi ya familia chini ya maagizo makali ya baba yake.


  Kama vile vijana wadogo waki Cape Verde, elimu ya sekondari ya cheka ililazimika kukatishwa kwasababu familia yake haikuweza kumudu gharama hivyo katika miaka yake ya ujana ilitumika katika uvuvi, kupiga mbizi pamoja na kutembea akichunguza maeneo katika kisiwa chake alipozaliwa.  Ilikua ni katika kipindi hiki ambapo alianza kutunga nyimbo. Akizungukwa na maumbo yenye mabonde bonde na yenye kuogofya ya milima ya Malagueta na bahari giza yenye mawimbi makali, Ribeira da Barca ilithibiti kua mandhari nzuri kabisa ambayo msanii anaweza kutengeneza muono wa kipekee.
  Kazi ya kwanza ya Tcheka ambayo haikua ikihusiana na muziki kiukweli ilikua ndio kitu kilichomuwezesha kuongeza upeo wake wa sanaa ya kimuziki. Mwaka 1991 akiwa na umri wa miaka 18, alipata ajira kama mpiga picha msaidizi katika kituo cha kitaifa (kinachofahamika sasa kama TNCV) katika mji mkuu wa Cape Verde, Praia. Kutoka mwaka 1991 hadi 2000, Tcheka alifanya kazi kama mpiga picha huku akipiga muziki katika kazi za usiku na marafiki zake kwenye baa ndogo ndogo, hoteli pamoja na migahawa. Rekodi yake ya kwanza Maân ba des des kumida da? [kutakua na mazao kipindi hiki?] ilionekana katika CD ya mkusanyiko  Cap Vert Les Enfant (1991) ambapo alikua bado akifanya kazi kama mpiga picha wa TNCV lakini kwa kificho alikua akioneka bado akifanya kazi yake hii ya muda wote.


  Sehemu kuu ya mabadiliko katika kazi yake ilikuja mwaka 2000 wakati alipotoa CD ya mkusanyiko Ayan: New Music from Cape Verde.  Moja kati ya michango mitatu aliyotoa Tcheka katika mradi huu wa aina yake ilikua ni aina ya mwanzo ya Primeru bes kin ba Cinema [Mara ya kwanza nilipokwenda sinema] ambapo anaelezea kwa mapana na marefu , mara yake ya kwanza alipoona filamu. Nyimbo hiyo haikua tu ikikumbushia wakati wa ghafla, wa kutisha na kutoweza kubadilishwa kwa kupotea kwa heshima kunakoletwa na njozi zenye kutongoza katika luninga, lakini pia inatambulisha kwa Tcheka muonekano huo kama dhima kuu na njia ya uwasilishaji wa tungo zake.  Tcheka anaelezea mchakato wa uundaji wake: ‘wakati natengeneza nyimbo, ni kama vile mtiririko wa picha, kama fremu za filamu mbele ya macho yangu. Mlio wenyewe ni hadithi ambayo naiona katika kichwa change kisha naandika mashairi kutokana  na picha hiyo’.  Kiukweli, kitu ambacho kwa haraka kinamtenganisha Tcheka na waandishi wengine wa Cape Verde ni hali ya kipekee na isiyofuata mtiririko maalum anayotumia katika kuunda nyimbo zake, mara nyingi kukiwa na mabadiliko ya ghafla katika kasi ya mapigo, mlio, mada katika mashairi na hisia, ikiashiria mikato ya haraka na mabadiliko ya picha kama ilivyo katika filamu.


  Toleo la Argui! [Get up] (2002), albamu yake alofanya mwenyewe, iliimarisha sifa yake Cape Verde kama mpiga gitaa maridadi na mwandishi orijino mwenye hisia na mafanikio yake alimfanya Tcheka afanye kazi ya muziki muda wote. Mwaka 2005 aliingia katika mashindano yenye sifa kubwa ya Radio France International Decouverte Musiques du Monde Competition yaliyofanyika Dakar, Senegal na kushindana na baadhi ya wasanii wanaoongoza katika Muziki wa kisasa wa Kiafrika.  Kama ada, alirudi nyumbani  Cape Verde na zawadi ya kwanza na mwishowe umaarufu wa kitaifa na wamataifa mengine.  Ilikua hata hivyo albamu yake ya Nu Monda (2005) iliyopata sifa nyingi ambayo ilimrusha anga ya juu katika muziki wa dunia  na kuacha ndimi zikitikisika  nyumbani pamoja na ughaibuni kuhusu yeye kua kiongozi katika muziki wa Cape Verde.


  Katika albamu yake, Lonji [mbali sana], Tcheka anaingia chini zaidi katika himaya ya majaribio. Akiwa na mpiga gitaa maarufu wa rock kutoka Brazil Lenine kama prodyuza, anabakia katika mitindo yake halisi yenye mahadhi yaki Afro-Creole huku akiongeza vionjo vya kielektroniki na zenye kuakisi mazingira yanayozipa nyimbo hizo upya na hali ya wakati ujao.  Baadhi ya mahadhi yaliyotumika katika rekodi zilizopita yanaimarishwa zaidi hapa: kuna hisia ile ya ubaridi na ya maji kwenye aina mpya ya Primeru bes kin ba Cinema; joto, hali ya uzito na msisimko wa Lingua Pretu [ulimi mweusi] na Ana Maria;  na hali ya kustaajabisha na yaki angahewa katika Lonji. Vile vile kuna msisitizo katika mikito ya ngoma katika rekodi hii; msuguano wakiutofauti waki Cape Verde, Afrika Magharibi na Afro-Brazil ambao wakati mwingine unakua mlaini, wenye kuchezeka na wakati mwingine, wenye nguvu kama radi. Kitu ambacho kimetunzwa kwa umakini , ni uandishi wa mashairi wenye kuleta picha unaowasilishwa na sauti ya Tcheka ambao bado hua inalia na ulaini na yenye kubembeleza.


  Bila shaka, Tcheka ni kijana mkuu wa sanaa ambayo ameivumbua na kama muongozaji mwingine yeyote, asili yake ni ngumu elewa ukiacha kuishikia chini.  Ikienda tofauti na maoni ya waandishi wa habari, yeye sio wa kisasa wala wa asili na muziki wake unazuia mgawanyo au mfananisho. Huku akifanya marejeo kutoka katika vipengele tofauti vya muziki wa ki Cape Verde (batuku, funana, finason, taganka, morna na coladera).  Muziki wa Tcheka pia ni makutano kati ya muundo wa kiCarribean, Brazil na Kiafrika , katika folk, jazz,blues,rock,fasihi,anthropolojia na filamu. Sio tu wa kiSantiago, sio tu waki Cape Verde na sio muziki tu. Labda kitu Tcheka anachokiwasilisha ni katika muonekano mpya kabisa kuhusu nini inamaanisha kuwa  mCreole katika zama za utandawazi: kuwa zao la muunganiko wa nguvu za kihistoria za utumwa, ukoloni na uhuru wa kitaifa, na wakati huo huo kua umeathirika na maendeleo baada ya maendeleo pamoja na kukua na kutoepuka safari na makutano ya mataifa tofauti kwa kuibuka kwa serikali mpya za kimawazo, sanaa na ubepari na kuongeza kutotenganisha teknolojia na uwezo wa mawazo wa binaadamu.
   

  learn_africa_logo
  with support from Learn Africa