4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: By Country > Sudan
Results: 2 to 2 of 2
  • Camirata Group

    Country  Sudan
    Genres roots traditional
    FestivalSauti za Busara 2012

    CAMIRATA

    Camirata Group
    Camirata Group

    Sudan ni nchi kubwa kieneo na kisiasa imeungana na Afrika na Urabuni. Sudan ni kitovu cha muziki kwa miaka kadhaa, na yenye historia ndefu ambayo imeunganisha nchi za jirani kama Misri, Eritrea, Ethiopia, Sudan ya kusini, Chad na Libya.

    Camirata Group ni wataalam wa ngoma za utamaduni nchini Sudan katika mji wa Khartoum. Dafaalla Elhag ni mpigaji wa vifaa tofauti na kiongozi wa kikundi ambaye mawazo yake ndio yalifanikisha kuzaliwa kwa kundi hilo, kwa kuunda kikundi cha muziki mwaka 1997.

    Walianza kutumia vifaa aina 8 na ngoma aina tofauti kutoka nchi nzima na watu watatu. Katika jitihada za kuliendeleza kundi lao walianzisha mafunzo kwa wasanii kwa kushirikiana na wanamuziki wengine na kufanikiwa kuongezeka idadi yao mpaka kufikia watu 15 pamoja na wachezaji.

    Kwa sasa bend inafanya maonyesho katika mji wa Khartoum ambapo lengo lake ni kufikisha ujumbe wa kutengeneza msingi wa umoja kupitia muziki. Kwa sasa ni moja ya kikundi ambacho kipo chini ya kituo cha muziki kijulikanacho kama Sudanese Traditional Music Centre kilicho chini ya Daffaalla. Lengo la kituo ni kutangaza na kufundisha muuziki, wanamuziki wa aina tofauti. Na pamoja na kuandaa matamsha mbalimbali, vilevile kituo kinafanya utafiti wa asili ya vyombo vya muziki wa asili na kukuza maisha ya amani kupitia muziki.

    Camirata wanapiga nyimbo kutoka kila sehemu ya Sudan kama “ Farsab” kutoka Sudan ya mashariki yenye kuchezwa na upanga. “Darb al Habib” ni nyimbo kutoka Kordofan magharibi mwa Sudan. “Jamal Jin” (mrembo mwenye haiba) ni nyimbo kutoka Darful na “Al Furag” yenye maana ya utengano ni kutoka Nubia kaskazini mwa Sudan. Vile vile wanapiga nyimbo kutoka kusini mwa Sudan kama “Konji Kwanj”.

    Tuna uhakika manyesho yao katika tamasha la Sauti za Busara litatupelekea hisia zetu kufurahia muziki wa Sudan kwa mchanganyiko wa zana muziki, uchezaji upigaji kutoka Sudan.

    bc-stacked-295-rgb
    With thanks to the British Council Sudan