4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: A - Z > B
Results: 2 to 2 of 29
  • Babawatoto Centre

    Country  Tanzania
    Genres acrobats
    Website babawatotofitforlife.net
    FestivalSauti za Busara 2015
    Babawatoto Centre
    Babawatoto Centre

    Kituo cha watoto cha Babawatoto Centre kilianzishwa mwaka 2006 Makurumla, katika kitongoji kinachoishi watu wengi jijini Dar es Salaam. Mwanzilishi ni Mr. Mgunga Mwa Mnyenyelwa, mtendaji maarufu wa sanaa za maonesho ambaye pia alianzisha shirika maarufu ya maonesho Parapanda Theatre. Babawatoto Centre ina lengo la kuwawezesha vijana na jamii zilizokandamizwa ili waweze kushinda changamoto mbalimbali kama za upendeleo wa kijinsia, umasikini, uhalifu na magonjwa. Babawatoto ina muono wa jamii yenye watoto huru na walio mbali na unyanyasaji Tanzania.
    Babawatoto ni shirika bunifu linatotumia njia shirikishi ikiwemo sanaa za maonesho na sarakasi. Zaidi ya watoto 80 wanashiriki katika sarakasi, sanaa ya trapezi, juggling na ngoma za samba reggae vimewaongezea uwezo ndani ya Babawatoto.
    Babawatoto hutumia sarakasi kama nyezo ya kutoa ufahamu kwa jamii kuhusiana na watoto wa mitaani. Maonesho ya kuigiza ya mtaani huvutia watoto kwenda Babawatoto Centre badala ya kucheza majalalani. Maonesho yao njia ya kipekee ya kuburudisha ambayo huburudisha watu wa rika zote na tamaduni tofauti.
     

    LOGO-CEFA--Eng-re-JPG
    with support from CEFA Tanzania