4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: A - Z > O
Results: 2 to 2 of 14
  • Octopizzo and band

    Country  Kenya
    Genres hiphop
    Website www.octopizzo.com
    FestivalSauti za Busara: 2015
    Recordings📼

    Chocolate City (2014); Blackstar (2014); Hala (2014); Youth (2014); Vile inafaa ft Muthoni (2013); So Alive (2013); Mama (2012); Ivo Ivo Ivo (2012)

    OCTOPIZZO - Ivo Ivo Ivo [ItsNambaNaneTV]

    Octopizzo and band
    Octopizzo and band

    Jina lake halisi ni Henry Ohanga aka Octopizzo, mzaliwa wa Kibera, moja ya makazi maskini makubwa Afrika, Octopizzo ni msanii ambaye yupo kwenye kasi kubwa ya kupanda kuelekea umaarufu. Mpenzi wa dhati wa hiphop, alishawishiwa kwa kiasi kikubwa katika miaka yake ya awali ndani ya Kibera. Akiwa na miaka 25, hutazamia wasanii halisi wa hiphop kama wanaompa ari kuu akiwemo KRS-one, Immortal Technique, Big L, EPMD, CL Smooth na wengineo.
    Octopizzo ametumbuiza pamoja na ma rapa wa ndani ya nchi na wa kimataifa wakiwemo Dead Prez, Burnt Face (Ethiopian American hip hop group), Wyre, Nonini, Jua Cali, Ukoo Flani, Jaguar na wengineo. Ameshinda mashindano tofauti ya freestyle Kenya ikiwemo G Pange Hip Hop Challenge, Hip Hop Halisi Freestyle Challenge, na Usanii Kona Hip Hop Challenge. Pamoja na kutumbuiza Uingereza, Ujerumani na Afrika Kusini, amefanya maonesho mengi Kenya ikiwemo WAPI (Words and Pictures), Sprite Challenge, Ghetto Radio Serious Request, Translating Hip Hop (Goethe Institut), International hip Hop Summit, Grand National peace Concerts, Global Development of Peaceful Environments na matamasha mengine kadhaa ya vyuo vikuu, misaada pamoja na ufahamu wa virusi vya UKIMWI.
    Hadi kufikia leo, Octopizzo amerekodi mixtape 3: S.O.N (Stragglers of Nairobi), Y.G.B (Young, Gifted and Black) na The White Shadow. Albam yake Chocolate City pia ipo kwenye iTunes.
    Octopizzo ni mshiriki mkuu katika jamii yake na muziki wake unaakisi hili, huku mashairi yake yakiwahamasisha waKenya kupiga kura, na hitaji la amani na uwiano wa kiuchumi. Ni mwanzilishi na Mwenyekiti wa shirika la jamii Young, Gifted and Black linalojumuisha ma rapa, washairi, wasanii wa michoro ya mtaani, wasanii wa grafiki na madansa.
    Octopizzo ni mjasiriamali, anasimamia mavazi ya YGB Wear, taasisi tofauti pamoja na uwezo nafasi za kuigiza chini ya himaya yake. Amekua kijana balozi wa mashirika kama UMaY (Uplifting Men and Youth in Africa) na Universal Peace Federation Kenya. Anaendesha Chocolate City Tours, kampuni ambayo ilimtembeza 50 Cent katika makazi maskini ya Kibera
    2012 ulikua mwaka mzuri kwa Octopizzo. Alichaguliwa kuwania Msanii wa Mwaka katika Kisima Awards na nyimbo yake On Top ilichaguliwa kuwani nafasi ya video bora ya Hip Hop. Alishinda nafasi ya Msanii Bora wa Mwaka 2012 katika tuzo za Coastal Nzumari Awards
    Kama vile wasanii wenzake katika tasnia ya muziki wa hiphop nchini Kenya, Octopizzo kwa kawaida hupiga muziki kwa kutumia ‘playback’ lakini hivi sasa yupo bize akijiandaa kutoa onesho nadra na maalum katika Sauti za Busara 2015, 100% live!