4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: Year > 2013
Results: 2 to 2 of 22
  • Burkina Electric

    Country  Burkina Faso Austria
    Genres fusion roots urban dance
    Website www.burkinaelectric.com
    FestivalSauti za Busara 2013
    Recordings📼

    Rêem Tekré, 2007; Paspanga, 2010

    Burkina Electric - "Sankar Yaaré" (DJ Spooky Remix)

    Burkina Electric
    Burkina Electric

    Burkina Electric ni bendi machachari katika tasnia ya muziki nchini Burkina Faso hasa kutokana na mseto wa wasanii wake na aina yao ya kisasa ya uchezaji, kundi hili lenye maskani yake mjini Ouagadougou lakini ni kundi la kimataifa kutokana na baadhi ya wanamuziki wake kuishi sehemu mbalimbali kama Marekani. Likiwa limesheheni vijana wenye vipaji na ubunifu wa kulishambulia jukwaa, na uchanganyaji muziki kutoka kila pande ya dunia.Midundo kama ya “Rock” na “Funk” ambayo Burkina Electric wanaongezea na vionjo vya umeme na kupata kitu adimu kabisa kuwahi kusikika Afrika.

     

     Maï Lingani mshindi wa tuzo ya uimbaji nchini Burkina Faso ambaya anaimba lugha tofauti kama Moré, Dioula, Bissa na kifaransa. Wende K. Blass  mpiga gitaa mashuhuri wa Burkina, Lukas Ligeti mpiga ngoma, mtunzi wa kimataifa na fundi umeme aliyehamishia makazi yake nchini Marekani, Vicky and Zoko Zoko wanaongoza safu ya uchezaji na uimbaji.

     

    Asili ya Burkina Electric ilianzia kwa Maï Lingani, Wende K. Blass na Lukas Ligeti ambao walikuwa marafiki wa karibu sana katika bendi Beta Foly. Kundi la Burkina lilianzishwa katika ziara ya kimuziki nchini Austria ambapo ushirikiano wao ulikuwa ni wa kuvutia na wakaamua kuendelea kama bendi kamili.

     

    Walitoa Cd yenye nyimbo nne “Rêem Tekré” na baadae kufanyia marejeo ya nyimbo zao na Dj Spooky, Paul de Jong of The Books, Rupert Huber kutoka Tosca, Badawi, na Mapstation. Mwaka 2010 walitoa albamu yao ambayo inapatikana dunia nzima, kupitia Lebo ya “New York label Cantaloupe Music”

     

    Burkina wameshafanya maonyesho matamasha mbalimbali kama Festival Jazz à Ouaga nchini Burkina Faso, Global Copenhagen nchini Denmark, Le Poisson Rouge nchini Marekani katika mji wa  “New York City”, The Old Town School of Folk Music nchini Marekani jijini Chicago, Turner Hall Ballroom mjini Milwaukee, the Newman Center mjini Denver, “The Cleveland Museum of Art, the Detroit Institute of Arts”, “The Luminato Festival”katika mji wa Toronto nchini Canada, na the Montréal Jazz Festival, Canada na mengineyo.

     

    GI_Logo_horizontal_green
    With thanks to Goethe Institut