4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: Year > 2015
Results: 12 to 12 of 36
  • Erik Aliana

    Country  Cameroon
    Genres acoustic roots fusion
    Website www.erikaliana.com
    FestivalSauti za Busara 2015
    Recordings📼

    Just My Land ( 2013); Songs from Badissa (2011); Just African (2006)

    Erik Aliana Kouroungangan

    Erik Aliana
    Erik Aliana

    Uelewa wa haraka na nguvu laini za Erik Aliana vimeweza kumpa hadhi kama msanii muhimu wa Kiafrika huko Ulaya. Akiishi hivi sasa Paris, Erik Aliana alikua kati ya vijiji viwili vya Yaounde na Badissa katikati mwa nchi ya Cameroon. Mgawanyiko wakitamaduni katika maisha yake uliweza kuanzisha uelewa wake katika muziki. Ufumaji wa bikutsi, kindo na makossa, uliokua ukipewa ari na mazingira ya Yaounde, sikukuu na sherehe za kimila za kijiji, sauti za mbilikimo na mabadiliko hisia ya msitu wa mvua, kazi za Erik Aliana zinaendeleza urithi tete na wakati huo huo ikizaa uzinduzi wa muziki mpya. Akitumia ala za asili kama vile mvet, balafon, sanza, eworo na vifaa vingine, kipaji chake kinawasilishwa katika mchanganyiko wa aina tofauti ya muziki na wakati akichanganya mahadhi ya asili na besi ya jazz, ikiwa na miguso ya fanki au cha cha. ..mashairi yake huimbwa katika ki Osananga, Kifaransa na Kiingerza ikionesha Afrika nzuri na iliyochangamka, vile vile ikiongelea mada za kisasa za jamii zinazochochewa na busara za kale.


    Erik Aliana, muimbaji, mpiga ala toufati anaheshimu, anaimarisha na kubadilisha tamaduni ya muziki wake wa asili kutoka Cameroon. Uwezo wake wa sauti yake maradufu hupaka rangi mitaa ya jiji kubwa ambapo anaishi hivi sasa, akiwa na mahadhi asili ya kijijini yakihimiza zogo hili la mjini. Ni katika makutano haya kati ya vijiji na jiji kubwa ambayo yanavutia uzuri, uthabiti na uwezo wa kiroho wa sanaa yake. Katika njia hii laini na yenye kuhitajia mengi, anasindikizwa vyema na kaka zake na wenzake wa Korongo Jam. Baada ya mwanzo wenye mafanikio Cameroon, Erik na kundi lake Korongo Jam walifanya ziara katika bara la Afrika. Mwaka 2003 wakati wa ziara yake kuu nchini Ulaya, kundi lake lilikua ni moja la ufichuo katika tamasha la Musiques Metisses, nchini Ufaransa. Mwaka 2005, Erik alifanya ziara nchini Marekani. Kat ya mwaka 2006 – 2009 alitumia muda Japan na Korea ambapo alikua mhusija mkuu katika Sukiafrika Sukiyaki Allstars, pamoja na mwimbaji na muandishi bora bora kutoka Zimbabwe Chiwoniso. Kwa pamoja walifanya ziara Afrika ikiwemo tamasha la Sauti za Busara mwaka 2011.


    Katika albamu yake ya kwanza Just African (2006) ilichangiwa na UNESCO na AFAA (Institut Francais). Mwaka 2011 ilikua mwaka ambao kwa mara ya kwanza alimishirikisha msanii mwingine, Buda Musique ambaye alitoa albam Songs of Badissa. Mwaka 2013, alirudi studio kurekodi Just My Land, moja ya albamu zake zilizopata umaarufu sana hadi leo.
     

    Terres-de-Musique
    With support from Terres de Musique