4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: Year > 2015
Results: 13 to 13 of 36
 • Ifa Band

  Country  Tanzania
  Genres acoustic
  FestivalSauti za Busara: 2015
  Recordings

  Chaguo Langu (2014)

  Ifa Band feat Totoo ze Bingwa - Chaguo lang

  Ifa Band
  Ifa Band

  Jafari Rashid Igomba ambaye ni mlemavu wa macho (kipofu), ndie mwanachama mwanzilishi wa Ifa Band. Mapenzi yake ya muziki ndiyo yaliyomvutia kutembelea mazoezi ya kikundi cha Baba Toni katika kijiji chake cha Ligama. Ni hapa ndipo alipojifunza kupiga gitaa. Mnamo mwaka 2000 bendi hiyo iliacha kutumbuiza na Jafari aliamua kuhamia katika wilaya ya Ifakara mkoa wa Morogoro, ambapo alikutana na marafiki ambao walikua wanavutiwa na muziki. Kwa pamoja waliunda bendi ya Ifa mwaka 2002 na wakaanza kutumbuiza katika maeneo tofauti mjini hapo. Ifa ni bendi inayohama hama kutoka sehemu moja kwenda nyingine kuburudisha watu popote ambapo wanaweza kulipwa. Ni bendi ya mtaani yenye vijana sita wa kiume, na muziki ndio njia yao pekee ya kuwapa kipato. Iliwachukua karibia mwezi mmoja kufika Dar es Salaam kutoka Ifakara, wakisimama na kupiga muziki wa kulipwa katika kijiji kimoja hadi kingine kwa vile hawakuweza kua na nauli ya kuwafikisha Dar es Salaam moja kwa moja.  Wakiwa wamelipiwa nauli ya kivuko kuja Zanzibar na vyumba vya hoteli vikiwa vimeshalipiwa mapema kwa ajili yao katika Sauti za Busara tuna uhakika wa kupata burudani ya muziki wa kusisimua.