4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: Year > 2015
Results: 14 to 14 of 36
  • Ihhashi Elimhlophe

    Country  South Africa
    Genres roots traditional
    Website www.mshiswamedia.com
    FestivalSauti za Busara 2015
    Recordings📼

    Siyabonga (2012); Isililo (2010)

    IHHASHI ELIMHLOPHE - UMVUMO

    Ihhashi Elimhlophe
    Ihhashi Elimhlophe

    Ihhashi Elimhlophe ni jina maarufu sana katika muziki wa kiZulu aina ya maskandi Afrika Kusini. Kiongozi Bheki Ngcobo, ndio akili nyuma ya kundi hili, mara ya kwanza kurekodi ilikua 1986. Hajawahi kuangalia nyuma kamwe.



    Mwaka 1976 Bheki Ngcobo alihama kijiji chake kidogo KwaZulu Natal kwenda Johannesburg kutafuta fursa. Alianza kazi yake ya muziki kama mpiga gitaa (bass) na Young Brothers. Alifanya kazi kwa muda na vikundi vingine kabla ya kujiunga na kundi maarufu la Soul Brothers. Waligundua kipaji chake kikubwa na kumfanya awe muimbaji mkuu wa kundi lao dogo , ‘Imitshotshovu’.



    Baada ya kurekodi albamu iliyopata mafanikio “icala”, Bheki aliamua kutafuta kazi kama msanii binafsi. Hapo ndipo aliamua kujipa jina la ‘Ihhashi Elimhlophe’ (Farasi Mweupe). Albamu yake ya kwanza “Hololo” ilifuatiwa muda mchache na kipindi kirefu cha kazi zenye mafanikio alizotoa. Hadi kufikia leo, familia ya Ihhashi imepanuka, ikiwemo Izintombi Zehashi, kikundi cha wasichana tupu, Amataliana, kikundi cha wanaume watatu na Amaponi, ikishirikisha watoto wa Ihhashi. Mke wake Linah Khama (aka “Ebony”) ni mmoja ya wanawake waimbaji maarufu wanaoongoza Afrika Kusini ambae amejitengenezea sehemu katika soko la muziki Afrika Kusini.

    Kuongezea katika mafanikio ya Ihhashi, alirekodi albamu shirikishi pamoja na wasanii wa kuheshimika wa maskandi, Phuzekhemisi na Mfazi Omnyma ambayo walijiita “Izingungulu Zomhlaba”.  Ushirikiano huu ulizalisha albamu mbili ambazo mara nyingi huingizwa katika mpangilio wa muziki wa DJ Yusuf kutoka Busara.



    Nyimbo za Ihhashi Elimhlophe zinatokana na hitaji la kufidhani tamaduni na urithi wa mtu na wakati huo huo kuendeleza upendo na amani kati ya watu wa Afrika Kusini’, anasema.
    Ihhashi Elimhlophe, mfalme wa maskandi, unakaribishwa sana Zanzibar!
     

    LOGO_1_CMYK-ON-WHITE
    with support from Concerts SA