4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: Year > 2013
Results: 20 to 20 of 22
  • Super Maya Baikoko

    Country  Tanzania
    Genres roots traditional
    FestivalSauti za Busara 2013

    KAYA BAIKOKO - NGOMA YA TANGA

    Super Maya Baikoko
    Super Maya Baikoko

    Baikoko ni ngoma inayojipatia umaarufu kila kukicha katika maeneo mengi ya jiji la Dar es
    Salaam. Ngoma ya baikoko hupiga kwenye bar, harusi na katika kumbi mbalimbali za burudani. Kijana aliyebuni mtindo wa kupiga kwenye kumbi za burudani ni Juma Hussein au maarufu kama “Maya”. Ngoma ya baikoko asili yake kutoka mkoa wa Tanga kutoka kwa kabila la Wadigo kwenye miaka ya 90. Baikoko imepatikana kutoka kwenye ngoma mbalimbali za Wadigo kama gita, chera na mdundiko. Baikoko hupigwa na vifaa kama Msondo (aina ya ngoma ndefu), manyanga, mabuyu, dogole (ngoma kubwa ambazo zinaongoza wachezaji)

    Jinsi ya uchezaji wake ilikuwa inachukuliwa kama ni ngoma ya wanawake tu ambayo hairuhusiwi kuonekana na wanaume, huchezwa pindi wasichana wanapokuwa wamefikia umri wa kuolewa.

    Baikoko mara ya kwanza ilipigwa na kundi lijulikanalo Bazoka katika maeneo ya kisosora mkoani Tanga. Maeneo ya vijijini vifaa vya baikoko huwa havibadilishwi lakini kwa mjini hubadilishwa mara kwa mara kutokana na upatikanaji wa vifaa, kwa mfano ngoma za mjini zinatengenezwa kutokana na plastiki.  

    Maya alikuwa muimbaji wa ngoma tofauti kijijini kwao Pangarawe. Alihamia Tanga mjini na kuwa kiongozi wa kundi la Bazoka katika miaka ya 90. Hatahivyo kundi liligawanyika kutokana na kutoelewana na Maya kuunda kundi gingine aliyelipa jina la Channel O pamoja na baadhi ya wasanii aliyekuwa nae akiwemo Kwini.

    Kundi la Channel 0 lilifanikiwa kushinda mashindano ya Baikoko yaliyofanyika mkoani Tanga katika miaka ya 2000. Mwaka 2009 kipindi cha Ramadhan Maya alikwenda Dar es Salaam kuishi kwa kaka yake kwasababu kipindi cha Ramadhan hakuwa na ratiba ya kufanya maonyesho. Alikusudia kufanya kazi  ili apate pesa kwa ajili ya sikukuu na nauli ya  kurudia Tanga. Siku moja katika matembezi yake aliona plastiki zimetupwa na akapatwa na wazo la kuanzisha kundi la baikoko jijini Dar es Salaam mara mwezi wa Ramadhan utakapoisha.

    Kaka yake alimsaidia kutafuta mahitaji zaidi na kuwaleta baadhi ya wasanii wenzake kutoka Tanga.  Baikoko ikafanikiwa kuliteka eneo lote la Magomeni na Maya na kundi lake la Dogo Dogo Star bila ya wao kutegemea. Mafanikio yao ya haraka yalileta mvutano usioepukika kwa baadhi ya wasanii kuanza kufanya kazi na vikundi vingine na ikafikia muda kundi likagawanyika.

    Baikoko inaendelea kujikusanyia umaarufu katika miji ya Dar es Salaam, Mombasa na kisiwani Zanzibar, Maya na rafiki zake wanaendelea na kufanya maonyesho kama Super Maya Baikoko.