4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: Year > 2013
Results: 21 to 21 of 22
  • Wanafunzi wa SOS

    Country  Zanzibar
    Genres roots traditional
    FestivalSauti za Busara 2012, 2013
    Wanafunzi wa SOS
    Wanafunzi wa SOS

    Huu ni mseto wa watoto yatima ambao wapo chini ya skuli ya Hermann Gmeiner iliyopo Zanzibar katika kijiji cha kulelea watoto yatima cha SOS.

    Watoto waliopoteza wazazi wao huchikuliwa na katika harakati za kuwapa malezi bora, elimu, afya na mafunzo jinsi ya kuishi na jamii tofauti ndani na nje ya zanzibar. Vili vile shule ina mpango madhubuti wa kuvilea vipaji vya watoto kwa kuwataka wawe huru kuchagua mchezo wanaoutaka.

    Shule ilianzisha darasa maalumu kwa ajili ya ngoma za utamaduni kutoka zanzibar na Tanzania ili kuviendeleza vipaji vyao.

    Mwaka 1991 kikundi kilianzishwa rasmi na vijana wapatao 18 wote wanafunzi wa SOS baada ya kuwa na kazi kubwa ya kuwachagua na baadae kufanikiwa kuwapata wakali zaidi na wanaendelea kutoa burudani ya nguvu ndani na nje ya zanzibar.

    Hucheza msewe ngoma ambayo maarufu Zanzibar kutoka katika kisiwa cha Pemba ambayo huchezwa katika sherehe mbali mbali kama kwenye harusi, mavuno na sherehe za serikali.

    Kama nilivyosema awali kikundi hiki ni mseto wa vipaji kwa kuthibitisha hili wameweza kutumia vifaa mbali mbali vya muziki kama ngoma mbalimbali, filimbi, masewe, manyanga na aina nyingine katika maonyesho yao.

    Katika ujumbe wao hupendelea kuiasa dunia kulisa usalama na amani kwa kuwa kupindi cha vita vya wenyewe kwa wenyewe watu ambao wenye hatari ya kupoteza maisha ni akina mama na watoto.